Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia leo January 27, 2025 Imetembelea na kutoa Elimu katika Maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Geita ambapo Timu imetembelea kata ya Buhalahala na kufanikiwa kutembelea shule mbili ikiwemo shule ya Sekondari Mwatulole na Shule ya Sekondari Fadhilibucha zote zikiwa katika kata ya Buhalahala.
Baada ya kufika katika shule hizo mbili wanafunzi pamoja na walimu wamefanikiwa kupewa elimu mbalimbali ya msada wa kisheria inayotolewa bure na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Jopo la Mawakili likiongonzwa na Mwakilishi kutoka wizara ya katiba na sheria Moses Matiko , Afisa wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia , Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Geita pamoja na viongozi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Geita.
Pia Jopo la Mawakili la Msaada wa kisheria wa Mama Samia limepata nafasi ya kufika katika Ofisi za kata ya Buhalahala na kusikiliza Migogoro ya wananchi katika kata hiyo ambapo Jopo hilo limekutana na Mh. Diwani wa kata hiyo Dotto Zanzui pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali za Mtaa wa Mwatulole.Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia leo January 27, 2025 Imetembelea na kutoa Elimu katika Maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Geita ambapo Timu imetembelea kata ya Buhalahala na kufanikiwa kutembelea shule mbili ikiwemo shule ya Sekondari Mwatulole na Shule ya Sekondari Fadhilibucha zote zikiwa katika kata ya Buhalahala.
Baada ya kufika katika shule hizo mbili wanafunzi pamoja na walimu wamefanikiwa kupewa elimu mbalimbali ya msada wa kisheria inayotolewa bure na Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Jopo la Mawakili likiongonzwa na Mwakilishi kutoka wizara ya katiba na sheria Moses Matiko , Afisa wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia , Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Geita pamoja na viongozi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Geita.
Pia Jopo la Mawakili la Msaada wa kisheria wa Mama Samia limepata nafasi ya kufika katika Ofisi za kata ya Buhalahala na kusikiliza Migogoro ya wananchi katika kata hiyo ambapo Jopo hilo limekutana na Mh. Diwani wa kata hiyo Dotto Zanzui pamoja na Viongozi mbalimbali wa Serikali za Mtaa wa Mwatulole.