………………………
Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa amewakumbusha na kuwashauri Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA) kuhusu ufanisi wa kazi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili Mamlaka hiyo iweze kuongeza ufanisi wa kazi zaidi.
Akizungumza katika uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi leo Jijini Dodoma Kwandikwa alisema Baraza lina nafasi kubwa ya kuishauri Mamlaka juu ya maslahi bora kwa Wafanyakazi.
“Naomba Mjadili changamoto mnazokutana nazo mahala pa kazi na katika utekelezaji wa mipango ili kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wananchi, pia mjadili kuhusu makisio ya mapato na matumizi ya Mamlaka”alisema.
Pia alitaka Baraza hilo lisaidie katika kuleta maelewano kazini kwani Rasilimali watu ni muhimu katika kusimamia Rasilimali zingine na mipango katika Taasisi.
“Lazima tufanye kazi kwa umoja ili tuweze kupiga hatua, kwahiyo uwepo wenu ni muhimu katika kujadiliana namna ya kuendeleza Taasisi kwa kushirikiana”alisema.
Pia Kwandikwa alisema Baraza liweke mazingira ya kuongeza tija kwa Watumishi wanaotimiza majukumu yao ambapo lengo ni kutambua mchango wao na kuuthamini.
“Watumishi pia watimize majukumu yao kwa weledi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa umma”alisema.
Katika hatua nyingine Kwandikwa amewataka wafanyakazi wa Mamlaka wafanye maandalizi juu ya ufunguzi wa Jengo la tatu la abiria.
“Endeleeni kufanya uchunguzi juu ya vihatarishi vinavyoweza kujitokeza baada ya kuanza matumizi ya jengo hilo,na mshirikishane na kudhibiti mapema vihatarishi hivyo”alisema.
Pia aliwataka Watumishi sekta ya Anga kufanya kazi kwa weledi ili kuboresha huduma za usafiri wa Anga ili kuongeza ushindani wa Kitaifa na Kimataifa.
Pia alisisitiza kuwa ni muhimu Watumishi wa Mamlaka kujitambua kuwa wanamchango katika kukuza pato la Taifa kutokana na huduma wanazotoa ambazo zina mchango Mkubwa katika ujenzi wa Taifa.
Awali Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi Julius Ndyamukama kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi aliainisha baadhi ya changamoto zinazoitatiza Taasisi kuwa ni maslahi duni kwa Wafanyakazi, uchache wa Wafanyakazi pamoja na nyenzo za ufanyaji kazi kama magari ya Zimamoto.
Ambapo Kwandikwa alisema “Serikali itafanyia kazi changamoto hizo ili kuhakikisha inaboresha sekta ya Usafiri wa Anga huku akitoa wa wito kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa huku akisisitiza Maazimio ya Baraza hilo yale ambayo yamekuwa changamoto yawe fursa ili yaweze kufanyiwa kazi.
Mkutano huo wa 23 wa Baraza kuu la Wafanyakazi utafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.
………………………Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa amewakumbusha na kuwashauri Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA) kuhusu ufanisi wa kazi na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili Mamlaka hiyo iweze kuongeza ufanisi wa kazi zaidi.Akizungumza katika uzinduzi wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Baraza la Wafanyakazi leo Jijini Dodoma Kwandikwa alisema Baraza lina nafasi kubwa ya kuishauri Mamlaka juu ya maslahi bora kwa Wafanyakazi.“Naomba Mjadili changamoto mnazokutana nazo mahala pa kazi na katika utekelezaji wa mipango ili kuhakikisha mnatoa huduma bora kwa wananchi, pia mjadili kuhusu makisio ya mapato na matumizi ya Mamlaka”alisema.Pia alitaka Baraza hilo lisaidie katika kuleta maelewano kazini kwani Rasilimali watu ni muhimu katika kusimamia Rasilimali zingine na mipango katika Taasisi.“Lazima tufanye kazi kwa umoja ili tuweze kupiga hatua, kwahiyo uwepo wenu ni muhimu katika kujadiliana namna ya kuendeleza Taasisi kwa kushirikiana”alisema.Pia Kwandikwa alisema Baraza liweke mazingira ya kuongeza tija kwa Watumishi wanaotimiza majukumu yao ambapo lengo ni kutambua mchango wao na kuuthamini.“Watumishi pia watimize majukumu yao kwa weledi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu za Utumishi wa umma”alisema.Katika hatua nyingine Kwandikwa amewataka wafanyakazi wa Mamlaka wafanye maandalizi juu ya ufunguzi wa Jengo la tatu la abiria.“Endeleeni kufanya uchunguzi juu ya vihatarishi vinavyoweza kujitokeza baada ya kuanza matumizi ya jengo hilo,na mshirikishane na kudhibiti mapema vihatarishi hivyo”alisema.Pia aliwataka Watumishi sekta ya Anga kufanya kazi kwa weledi ili kuboresha huduma za usafiri wa Anga ili kuongeza ushindani wa Kitaifa na Kimataifa.Pia alisisitiza kuwa ni muhimu Watumishi wa Mamlaka kujitambua kuwa wanamchango katika kukuza pato la Taifa kutokana na huduma wanazotoa ambazo zina mchango Mkubwa katika ujenzi wa Taifa.Awali Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mhandisi Julius Ndyamukama kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi aliainisha baadhi ya changamoto zinazoitatiza Taasisi kuwa ni maslahi duni kwa Wafanyakazi, uchache wa Wafanyakazi pamoja na nyenzo za ufanyaji kazi kama magari ya Zimamoto.Ambapo Kwandikwa alisema “Serikali itafanyia kazi changamoto hizo ili kuhakikisha inaboresha sekta ya Usafiri wa Anga huku akitoa wa wito kufanya kazi kwa bidii na weledi mkubwa huku akisisitiza Maazimio ya Baraza hilo yale ambayo yamekuwa changamoto yawe fursa ili yaweze kufanyiwa kazi.Mkutano huo wa 23 wa Baraza kuu la Wafanyakazi utafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.