Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa  kushirikiana na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya  ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya mazingira, Jinsia na  Utetezi Pemba (PEGAO) tuna furaha kutangaza rasmi uzinduzi wa Tuzo ya uwiano  wa kijinsia kwa Vyombo vya Habari “Media for Gender Equity Awards” yenye  ujumbe unaosema “Kalamu Yangu, Mchango Wangu kwa Wanawake.” Tuzo hii  itatambua vyombo vya habari na waandishi wa habari Zanzibar vinavyoandika habari  za kina kuhusu mafanikio, changamoto, michango ya wanawake katika uongozi, na  vinavyoshiriki kikamilifu katika kukuza usawa wa kijinsia kupitia kazi zao. 

Malengo ya Tuzo  

Kupitia tuzo hii, TAMWA ZNZ inalenga kuhamasisha vyombo vya habari na waandishi  wa habari kuunga mkono sauti za wanawake na kukuza uandishi wa habari wenye  kuzingatia usawa wa kijinsia ili kuchangia mabadiliko ya kijamii kwa kuonesha nafasi  za wanawake na uwezo wao katika uongozi ili kuleta maendeleo. 

Utambuzi wa vyombo vya habari: 

Mara hii tuzo hizi zinalenga zaidi kutambua vyombo vya habari vyenye mtiririko mzuri  wa kusaidia kuongeza wanawake katika nafasi za uongozi. Hivyo vigezo  vitakavyotumika ni kuwa na sera ya kijinsia, dawati la kijinsia, zana za tathmini na  ufuatiliaji wa masuala ya usawa wa kijinsia, idadi ya habari zilizoandikwa kuhusu 

wanawake na uongozi na nafasi ya wanawake waandishi wa habari katika chombo  cha habari. Mradi wa SWIL uliwahi kuwapa mafunzo na kusaidia vyombo vya habari  

 @TAMWA_Zanzibar www.tamwaznz.or.tz  

11 kutoka Unguja na Pemba kuandika na kuweka kumbukumbu na kufanya ufuatiliaji  na tathmini katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2023. Hivyo tunaamini kuna vyombo  vimeweza kuleta mabadiliko makubwa na vinahitaji kutambuliwa na kuthaminiwa.  

Tunzo hii itahusisha kazi zilizotolewa na waaandishi wa habari katika  vyombo vya habari vya aina nne (4) kama ifuatavyo: 

Uandishi wa habari za Makala katika magazeti (feature articles). 

Uandishi wa habari wa vipindi katika redio (radio program). 

Uandishi wa habari katika Televisheni (TV program). 

Uandishi wa habari wa makala katika mitandao ya kijamii (feature articles in social  media story). 

Vigezo muhimu vya kuzingatia ni; 

∙ Ubora wa kazi iliyowasilishwa. 

∙ Upekee wa mada. 

∙ Umuhimu wa kuzingatia uwiano sawa wa jinsia. 

∙ Vyanzo vingi vya habari vilivyojitawanya. 

∙ Ubunifu wa mada husika. 

∙ Matokeo baada ya kutoka habari au kipindi hicho (impact). 

∙ Uwasilishaji wa mada husika. 

∙ Mpangilio wa mada. 

∙ Ufasaha na mtiririko wa lugha. 

∙ Kuzingatia maadili ya uandishi wa habari. 

∙ Uweledi na matumizi ya TAKWIMU. 

Kipindi cha Redio na Television kisizidi dakika 30 na pia sauti na picha ziwe katika  ubora unaostahiki. 

Kipindi au makala iliyochapishwa au kurushwa HEWANI katika vyombo mbali  mbali vya habari vikiwemo magazeti, runinga, redio na mitandao ya kijamii katika  kipindi cha kuanzia Januari 1 hadi Disemba 31, 2024. 

Kama ilivyokuwa kwenye vyombo vya habari SWIL pia ilikaa na waaandishi wa habari  170 kwa mafunzo na majadiliano kuhusu kuandika habari nzuri za wanawake na 

 @TAMWA_Zanzibar www.tamwaznz.or.tz  

uongozi. Kiasi cha waandishi wa habari 45 wametambuliwa kwa kuandika habari za  kuongeza ushiriki wa wanawake kuanzia 2021 hadi 2023.  

Mchakato wa Uwasilishaji na Vigezo vya Tathmini  

Dirisha la kupokea kazi liko wazi kuanzia kwa waandishi wa habari kutoka vyombo vya  habari mbalimbali Zanzibar, ikiwemo magazeti, televisheni, redio, na mitandao ya  kijamii. Jopo la majaji, likiwa na wataalamu wa uandishi wa habari na utetezi wa  kijinsia, litapitia kazi za vyombo vya habari na za waandishi wa habari mapema Januari  baada ya kukamilika kwa zoezi la ukusanyaji kazi.  

Maombi yamefunguliwa leo na kazi zitaendelea kupokelewa hadi tarehe 5 Januari,  2025. Waandishi wa habari wanaweza kuwasilisha kazi zao ambazo zimezalishwa  kuanzia Januari hadi Disemba, 2024 moja kwa moja Ofisi za TAMWA ZNZ zilizopo  Tunguu na Mkanjuni Chakechake Pemba, au kupitia barua pepe ya  [email protected] na kiungo/link itakayotumwa kwenye mitandao ya kijamii. 

Hitimisho  

Tunawakaribisha waandishi wa habari na vyombo vya habari kushiriki katika tuzo hizi  muhimu, ili habari zenu ziwe ushahidi wa nguvu ya uandishi wa habari katika kuleta  mabadiliko chanya. Kwa maelezo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia [email protected], & [email protected]. 

Tuzo hizo ambazo ni mara ya nne kufanyika zinafanywa kupitia mradi wa Kuwajengea  Wanawake Uwezo katika Uongozi (SWIL) kwa mashirikiano na Ubalozi wa Norway. 

 @TAMWA_Zanzibar www.tamwaznz.or.tz