Mtendaji Mkuu wa SAAOK Bw.Zine Laroussi(Kushoto) akimuonesha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara .Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya picha za miradi wanayotekeleza kwenye nchi mbalimbali za Afrika.
Picha ya Pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara,Watendaji wa Kituo cha Biashara cha Slovakia,Afrika na Uarabuni(SAAOK) na maafisa wa Wizara na Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara waliohudhuria kikao hicho.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara .Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya akizungumza na Watendaji wa Kituo cha Biashara cha Slovakia,Afrika na Uarabuni(SAAOK) na maafisa wa Wizara na Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara waliohudhuria kikao hicho.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara .Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya akifafanua Jambo wakati wa kikao na Watendaji wa Kituo cha Biashara cha Slovakia,Afrika na Uarabuni(SAAOK) na maafisa wa Wizara na Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
****************************************
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Eng. Stella Martin Manyanya (Mb.) leo Jijini Dar es Salaam amewataka wawekezaji kutoka Kituo cha Biashara cha Slovakia,Afrika na Uarabuni(SAAOK) kufanya uwekezaji utakao kuwa na manufaa kwa wazalishaji wa bidhaa za Viwanda nchini.
Akizungumza na Watendaji wa Kituo hicho kwenye kikao kilicholenga kuwaelezea fursa za uwekezaji zinazopatika hapa nchini Mhe.Manyanya amesema bado Tanzania inahitaji wawekezaji kwenye sekta ya mifugo ili kuboresha bidhaa za ngozi.
“Tanzania ina ng’ombe milioni 50,ni idadi kubwa lakini ufugaji wake sio wa kuzingatia ubora malighafi zinazohitajika kuzalisha bidhaa za ngozi zenye kiwango cha kimataifa.Kwahiyo uwekezaji kwenye sekta ya mifugo utahakikisha upatikanaji wa malighafi zenye ubora wa kimataifa kwa ajili ya Viwanda vya bidhaa za ngozi”.
Pia amewataka kuwekeza kwenye Viwanda vya kutengeneza mashine zikazowasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kusaidia uchakataji malighafi ili kuziongezea thamani.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa SAAOK Bw.Zine Laroussi amesema kituo hicho kinafanya miradi mbalimbali kwenye nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na Nishati,Maji,Chakula,Elimu,Usafirishaji na kutoa Misaada ya Kibinadamu kwa lengo la kuboresha hali za maisha ya watu.
Bw.Laroussi amesema kwa mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwa ni pamoja na Algeria wamekuwa wakishirikiana na jamii kubaini changamoto zinazowakumba kisha wanaziwezesha kifedha na kitaalam kukabiliana na changamoto hizo.