Mratibu wa bidhaa na huduma za kidigitali wa Bank of Africa Tanzania, Bw Fortunatus Joachim (Kulia) akimkabidhi zawadi ya simu janja ya kisasa aina ya I-phone 15 kwa mshindi wa droo ya pili ya kampeni ya matumizi ya huduma za kidigitali inayoendeshwa na benki hiyo Samira Ayubu Msangi wa tawi la NDC, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
……………..
Mteja wa Bank of Africa Tanzania tawi la NDC jijini Dar es Salaam, Samira Ayubu Msangi, ambaye aliibuka mshindi  wa pili wa zawadi katika droo ya pili ya kampeni ya Kigitali ijulikanayo kama “Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15 inayoendeshwa na benki hiyo amekabidhiwa zawadi yake ya ushindi ya simu aina ya I-phone 15. Droo ya kumpata mshindi  ilisimamiwa na Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha.

Kampeni ya “Ingia B-Mobile utoke na Iphone 15” ilianza Juni 10, 2024 na itaendeshwa kwa miezi 3 na wateja wengine wenye bahati wataweza kujishindia simu janja za  kisasa aina ya I-phone 15. Ili kushiriki kampeni  wateja wa Bank of Africa, wanatakiwa kufanya miamala ya  kidigitali kupitia programu ya Benki ya simu ya kiganjani (B-Mobile) au kwa kupiga (*150*13#) kufanya miamala mingi iwezekanavyo na kutoa pesa kupitia WAKALA wa BOA ili kuingia kwenye droo inayofanyika kila mwezi.

Akiongea wakati wa droo hiyo,Mratibu wa bidhaa na huduma za kidigitali wa Bank of Africa, Bw Fortunatus Joachim,  alisema kampeni hii imelenga kuwezesha wateja wa Benki  kutumia mfumo  wa kidigitali kupata huduma za kibenki ambao umeboreshwa kutumia simu ya kiganjani kukidhi mahitaji yao.

“Kama benki tumedhamiria kutoa bidhaa na huduma bora zinazokidhi mahitaji ya wateja. Benki itaendelea kukuza na kuleta mawazo mapya ya ubunifu kwendana na kasi ya ukuaji wa matumizi ya kidigitali katika tasnia ya benki  kwa ajili ya kukuza zaidi ajenda jumuishi ya kifedha,” alisema Bw.Fortunatus.

Mkuu wa Mawasiliano na Masoko, Nandi Mwiyombella, alisema : “Kupitia kampeni hii, wateja wetu na wapya wanaotumia huduma za benki mtandao (Mobile Banking) wataingia katika droo iwapo watafanya miamala kwa njia ya kidigitali na kutoa fedha angalau mara moja kutoka BOA  WAKALA.

Kampeni hii ni kielelezo cha lengo la kimkakati la benki kuweka bidhaa na huduma zake katika mfumo wa kidijitali na hivyo kukuza ushirikishwaji wa kifedha pamoja na urahisi wa wateja kupata huduma za benki.