Mkurugenzi wa Habari maelezo Zanzibar Juma Mohamed akibadilishana mawazo na Mmoja kati ya Wanadiaspora Maggid Mjengwa katika Ziara ya Wanadiaspora katika Sehemu mbalimbali ikiwemo shamba la Viungo(Spice)na kuangalia Wanyama Jozani Mkoa wa Kusini Unguja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi (Gavu)akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na ziara ya Wanadiaspora katika Sehemu mbalimbali ikiwemo shamba la Viungo(Spice)na kuangalia Wanyama Jozani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mtembezaji wageni katika Shamba la Kitundu Spice Rashid Ahmada Said akiwagawia wanadiaspora Mbegu za Mti wa Mdalasini wakati walipofika katika shamba hilo la Viungo (SPICE)wakiwa katika Ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali Zanzibar.
Wanadiaspora wakiwa katika ziara ya kutembelea sehemu mbalimbali za Vivutio vya Utalii Ikiwemo Viungo(Spice)Kitundu na kuangalia Wanyama Jozani Mkoa wa Kusini Unguja.
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.