Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia viongozi pamoja na wageni mbalimbali walioshiriki hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 03 Julai, 2024.
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akihutubia viongozi pamoja na wageni mbalimbali kabla ya kufungua Rasmi Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 03 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta utepe pamoja na mgeni wake Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi kuashiria uzinduzi wa Mwandoro Square katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 03 Julai, 2024.
Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mwandoro Square katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 03 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi zawadi ya mlango wa Zanzibar (Zanzibar Door) kabla ya ufunguzi Rasmi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 03 Julai, 2024.
Baadhi ya Wageni mbalimbali pamoja na Viongozi waliohudhuria ufunguzi Rasmi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) tarehe 03 Julai, 2024.