Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama
Janeth Magufuli wamejumuika pamoja na waumini wengine wa
Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza katika
Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyoongozwa na
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu
Renatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikusanya Sadaka ya
Ujenzi wa Kanisa katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya
Majilio iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya
Bugando jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini
wa Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza
katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyoongozwa na
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu
Renatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Askofu Mkuu
wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande
leo tarehe 8/12/2019.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza
Mhashamu Renatus Nkwande akihubiri katika Misa Takatifu ya
Dominika ya pili ya Majilio iliyofanyika katika Kanisa Kuu la
Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza leo tarehe 8/12/2019.
PICHA NA IKULU