**********************************************
Katika kuelekea sikukuu ya Eid El fitr Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limejipanga
kikamilifu kuhakikisha wakazi wa Mkoa wa Mbeya, wageni na wakazi wa mikoa jirani wanasherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu.
Kwa kutambua kuwa Mkoa wetu unapakana na nchi jirani ya Malawi pia barabara kuu inayounganisha nchi yetu na nchi jirani pamoja na mikoa jirani imepita hapa,
tumejipanga vizuri kuhakikisha usalama kwa watumiaji wa barabara wakiwemo
madereva na watembea kwa miguu. Wito wangu kwa watumiaji wote wa barabara kuzingatia sheria, alama na michoro ya usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Kuelekea kipindi hiki cha sikukuu, waumini wa dini ya kiislamu ushiriki katika sala kwa nyakati tofauti kulingana na ratiba zao, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha ulinzi na usalama katika misikiti.
Aidha ninatoa wito kwa viongozi katika misikiti kuhakikisha
wanaweka utaratibu mzuri hasa katika suala la ulinzi kwa kutumia kamati za ulinzi na usalama zilizopo ili kuhakikisha ulinzi maeneo ya ndani na nje ya misikiti.
Pia ninatoa rai kwa wamiliki wa kumbi za starehe kufuata sheria hasa kuzingatia leseni zao za biashara zinavyowaelekeza ikiwa ni pamoja na kuzingatia muda wa kufungua na kufunga sehemu zao za biashara, wenye kumbi za muziki kuhakikisha kambi zao zinaingiza idadi ya watu inayohitajika [capacity] pamoja na kuweka walinzi katika maeneo yanayowazunguka.
Wito wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla
kuzingatia ulinzi wa watoto, na pia kuwasaidia watoto hasa kuwavusha katika maeneo tete kama vile kwenye vivuko vya watembea kwa miguu barabarani au maeneo yenye mito ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.
Pia ili kuepuka watoto kupotea katika kipindi cha sikukuu, wazazi na walezi wanapaswa kuongeza umakini zaidi katika uangalizi wa watoto wao kila mahali watakapokwenda iwe ni makanisani, misikitini au katika maeneo yenye michezo ya watoto.
Pia tunasisitiza ulinzi na usalama katika makazi yetu, kuhakikisha kwa wale wanaotoka kuacha waangalizi katika makazi pia kuhakikisha tunajilinda kwa kufunga milango na madirisha ili kuepuka uhalifu katika nyumba zetu.
Aidha nasisitiza utoaji wa taarifa za uhalifu na wahalifu kupitia namba za simu
zifuatazo:-
RPC…………………………………………………………….0715 009 931
RCO…………………………………………………………… 0658 376 052
STAFF OFFICER…………………………………………….0658 376 006
OPERATION OFFICER……………………………………..0754 466 924
RTO…………………………………………………………….0658 376 472
OC FFU…………………………………………………………0658 376 009
OCD MBEYA…………………………………………………0659 884 996
OCD MBALIZI………………………………………………..0655 248 381
OCD CHUNYA……………………………………………….0655 248 381
OCD MBARALI………………………………………………0659 885 948
OCD RUNGWE………………………………………………0659 885 253
OCD KYELA…………………………………………………0659 887 919