Meneja wa kiwanda cha TDL,Aranyaeli Ayo Akiongea Katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Meneja Masuala Endelevu wa TBL,Irene Mutiganzi Akiongea Katika hafla hiyo.

Meneja wa kiwanda cha TDL,Aranyaeli Ayo, akikabidhi mascada kwa Naibu Kamishna wa Polisi,Afwilile Mponi 

Wawakilishi wa shule za sekondari zilizopata msaada wa printer kutoka TDL wakizipokea Katika hafla hiyo

 ……………….

Kampuni ya Tanzania  distilleries limited,maarufu kama Konyagi, chini ya kampuni ya TBL Group, imetoa msaada wa Printer kwa shule za sekondari jijini Dar es Salaam na jeshi la polisi,  ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na taasisi hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii hususani katika kuboresha sekta ya elimu nchini.


Hafla ya kukabidhi msaada msaada huo ilifanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Maofisa wa Polisi,walimu na baadhi ya wafanyakazi  wa TDL.

Wawakilishi kutoka taasisi zilizopatiwa msaada walishukuru kampuni hiyo kwa jitihada mbalimbali ambazo imekuwa ikifanya kukabiliana na changamoto za kijamii.Shule zlizopatiwa msaada huo ni sekondari ya Charambe,Sekondari  ya Kichanga, Tuangoma, na Pendamoyo

Akiongelea msaada huo, Meneja wa Masuala Endelevu wa TBL, Irene Mutiganzi, alisema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi nyingine za maendeleo kushirikiana kupambana na changamoto mbalimbali kwenye jamii, hususani katika sekta ya elimu kama ambavyo inaendelea kutoa msaada wa Printer na vifaa vya kurahisisha elimu mashuleni.