Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akizungumza jambo wakati akifungua Kongamano la Wahariri wa vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi Maafisa Mawasiliano/ Masoko na Wahariri, kutumia kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla.
wenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari, wa Kongamano hilo, Bw. Ben Mwang’onda, akimkaribisha Mgeni rasmi wa Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (hayupo pichani), kufungua kongamano hilo lililoandaliwa na Wizara hiyo ambalo linafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, mkoani Morogoro.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, akionesha chapisho la 19 la Ripoti ya Benki ya Dunia ya Hali ya Uchumi ya Mwaka 2023, (Tanzania Economic Update-The Efficiency and Effectiveness of Fiscal Policy in Tanzania, wakati wa Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, lililoandaliwa na Wizara hiyo mkoani Morogoro, ambapo amewaelezea jinsi chapisho hilo linavyoonesha namna Tanzania inavyofanya vizuri katika maeneo mengi yaliyofanyiwa utafiti ikiwemo kuimarika kwa hali ya uchumi, mwenendo mzuri wa utoaji wa fedha kwenda kwenye miradi ya maendeleo, nchi kuwa na hifadhi ya fedha za kigeni za kutosha, kuimarika kwa ukusanyaji wa kodi za ndani, mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara pamoja na usimamizi mzuri wa Deni la Serikali na kushauri mambo kadhaa ikiwemo uimarishaji zaidi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kupitia kodi za ndani, usimamizi bora zaidi wa Bajeti Kuu ya Serikali na huduma nyingine za jamii.
Baadhi ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, alipofungua Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kutumia kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla.
Meneja Masoko na Uhusiano kwa Umma – PSPTB, Bi. Shamimu Mdee (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Shirika la Bima la Taifa (NIC) Karimu Meshack (wa pili kulia) na Meneja Masoko na Mawasiliano kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Amani Nkurlu (wa pili kushoto), wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya Fedha, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine wamepata fursa ya kuelezea mafanikio na miradi mbalimbali ya taasisi zao kwa wahariri hao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa vitengo vya Mawasiliano/ Masoko, kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, baada ya kufungua Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha, ambalo limeandaliwa na Wizara ya hiyo, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kutumia Kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla. Kulia walioketi ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja na Mwenyekiti wa Wahariri wa Vyombo vya Habari wa Kongamano hilo Bw. Benny Mwang’onda.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo (katikati walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari, baada ya kufungua Kongamano la Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wakuu wa Vitengo vya Mawasiliano kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha ambalo limeandaliwa na Wizara ya hiyo, mkoani Morogoro kwa siku mbili kuanzia tarehe 25 hadi 26 Oktoba, 2023, ambapo pamoja na mambo mengine amewasihi kutumia Kongamano hilo kujadili na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya Mawasiliano ya Umma na usambazaji wa taarifa, kwa ustawi wa Taifa kwa ujumla. Kulia walioketi ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja na Kushoto ni Mwenyekiti wa Kongamano hilo la Wahariri, Bw. Ben Mwang’onda.
……………………………………