Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto,akiwaonyesha watuhumiwa waliokamatwa kwa kuingia nchini kinyume cha Sheria
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto,akionesha fedha milioni moja kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo watuhumiwa walijaribu kuwarubuni Askari kwa kutoa rushwa.
……………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia Raia wanne kutoka
nchini za Somalia na Ethiopia Kwa kuingia nchini bila kibali huku pia
likiwashikilia watu wawili Raia wa Tanzania waliokuwa wakiwasafirisha wahamiaji haramu hao .
Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma,Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema mnamo tarehe 23,10,2019 majira ya saa 10:00 huko katika kijiji na kata ya Mtera Tarafa ya Rudi Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma ,walikamatwa wahamiaji haramu wanne walioingia nchini bila vibali.
Kati yao ,Wawili ni Raia wa Ethiopia na Wawili ni Raia wa Somalia
huku pia wakikamatwa watanzania wawili waliokuwa wakisafirisha
wahamiaji haramu hao kutoka Arusha Kwenda Iringa kwa Kutumia Usafiri wa pikipiki mbili .
Waliokamatwa ni Sellamu Yohanes[24] Raia wa Ethiopia,Ashetu
Tesfaye[20]Raia wa Ethiopia,Mahamoud Mapaa[19]Raia wa Somalia,Cuse Ciise [18]Raia wa Somalia .
Kamanda Muroto amewataja Raia wa Kitanzania waliokuwa wakiwasafirisha wahamiaji haramu hao kwa kutumia pikipiki ni Jamali Babuu Martin [26] dereva wa bodaboda ,mkazi wa Orasite Arusha akiendesha pikipiki namba MC 942 AXK KINGLION Chassis Na.LTBPK8BG5F2KO9729 rangi nyeusi.
Mwingine ni Wiston Alex Makia Ally [25] Dereva wa Bodaboda mkazi wa Mbauda Arusha akiendesha pikipiki Na.MC 767 CEB Dayun Chassis Na.L7GPCJLYH1099156 rangi nyeusi.
Kamanda Muroto ametaja mbinu waliyotumia kuingia nchini ni kwa
kutumia usafiri wa pikipiki kuvuka mipaka na vizuizi vya barabarani.
Aidha ,amebainisha kuwa watuhumiwa walijaribu kuwarubuni askari kwa kutoa rushwa ya Tsh. Milioni moja [1,000,000/=] ili waweze kuachiliwa na wakati wanakamatwa walikuwa na pesa Tsh.laki tano[500,000/=] lakini askari walikataa hongo ya rushwa hiyo na waliwakamata pamoja na pesa yao na kuwafikisha kituoni na watafikishwa mahakamani.
Katika hatua nyingine kamanda Muroto amesema Jeshi hilo limekamata nyara za Serikali ambapo mnamo Tarehe 21,10,2019 majira ya saa 1:30 jioni huko kijiji na kata ya Mkoka Tarafa ya Zoisa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma alikamatwa STEPHANO MTAGWA KOGANI[39] Mkazi wa kijiji cha Songambele na Hamis Mathayo Mabuku [45] na mkazi wa kijiji cha Matongolo Wakiwa na pembe moja ya tembo ndani ya mfuko wa Salfeti kiroba kinyume cha sheria na watafikishwa mahakamani upelelezi
ukikamilika.
Tukio jingine Kamanda Muroto amesema ni la kuvunja nyumba mchana na kuiba ambapo amekamatwa Elias Shaban Joseph [21]Mkazi wa Mailimbili Mnadani baada ya kuvunja nyumba mchana na kuiba maboksi 8 ya mafuta ya kupaka na maboksi 4 ya pipi mali yenye thamani ya TSH.720,000 Maeneo ya Ipngala West Dodoma mali ya Willy Fidelis Mgeni huku pia wakikamatwa wengine walioshiriki uhalifu huo .
Hata hivyo,Kamanda Muroto ameipongeza vyombo vya habari kwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuuhabarisha umma.