BODIya Usimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania (Gaming Board of Tanzania, GBT)
imefanikiwa kutwaa TUZO ya mshindi wa kwanza (First winner prize) katika kundi
la Mamlaka za Usimamizi (Regulatory Bodies) katika Maonesho ya 47 ya Biashara
ya Kimataifa ya Dar es Salaam yaliyofikia kilele Julai 13, 2023.
TanTrade
iliweka utaratibu mpya wa namna ya kumpata mshindi ambapo mwaka huu wananchi ndio
waliopewa fursa ya kuchagua mshindi kwa kupiga kura kupitia mtandao tofauti na
miaka ya nyuma ambapo kamati maalum ilikuwa ikipita kwenye mabanda kisha kuchagua
washindi.
“Sisi
tunachukulia haya ni mafanikio makubwa sana kwetu na tunawashukuru Watanzania
kwa kututambau na kuthamini kazi nzuri inayofanywa na Bodi ya Michezo ya
Kubahatisha Tanzania GBT.” Alisema Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe
wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Alisema
Wananchi wanatambua mchango wa sekta ya michezo katika maendeleo ya nchi.
“Katika
mwaka huu w afedha ulioshia Juni 2023 kiasi cha shilingi bilioni 160 za kodi ya moja kwa moja zitakusanywa kutoka kwenye sekta ikiwa ni ongezeko la kiasi cha shilingi
bilioni 148 zilizokusanywa katika mwaka wa fedha uliopita 2022.” Alifafanua.
Alisema
GBT itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu
zilizopo. “Michezo ya kubahatisha ni burudani sio ajira, ni ajira kwa
waendeshaji lakini ni burudani kwa wachezaji.” Aliwaasa washiriki wa michezo
ya kubahatisha.
Alisema
GBT imefikisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake na kadiri muda unavyokwenda ndivyo
imekuwa ikiimarika zaidi.
Aidha
akifafanua zaidi kuhusu tuzo, Afisa Uhusiano Mwandamizi GBT, Zena Athumani
amesema mbali na kupata tuzo hiyo ya mshindi wa kwanza kundi la Mamlaka za
Usimamizi, GBT pia ilitwaa tuzo ya mshindi wa tatu wa Banda bora la Maonesho
mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe akionyesha tuzo hiyo