Dk. Peter Kisenge Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya KIKWETE (JKCI) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mhandisi Peter Ulanga wakati alipotembelea banda la Shirika hilo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa  katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
(PICHA NA JOHN -BUKUKU)
…………………………………………..
Na Sophia Kingimali
Akizungumza Leo July 2 kwenye maonyesho ya 47 ya biashara Saba Saba jijini Dar es salaam Dk. Peter Kisenge Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya KIKWETE JKCI alipotembelea Banda la Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL amesema  uwepo wa Teknolojia hiyo
kurahisisha huduma Kwani wanaweza kuongea na mgonjwa popote anapokua na kumsaidia.
Amesema TTCL imefunga mtandao huo unaofahamika kama Tiba mtandao katika hospitali zote nchini hiyo imefanya kumfikia mgonjwa Kwa wakati na kumsaidia
“Hii huduma imetusaidia sana madaktari Kwani tunaweza kuwasiliana na mgonjwa na kuongea nae huku unamuona hata kama anakipele una kiona  na akisema maumivu unakua unamuona unajua jinsi ya kumsaidia”amesema Dk.Kisenge
 Kwa upande wake Afisa Muandamizi Shirika la Mawasilino Tanzania TTCL John Yahaya amesema  mpango wa uimarishaji wa mifumo ya inteneti yenye kasi ya juu katika mfumo wa tiba mtandao  umelenga kuboresha huduma.
Amesema, hatua hiyo inamuwezesha  daktari kuhudumia mgonjwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
“ Mbali na kupunguza msongamano katika upatikanaji wa huduma  inaunganisha watu kutoka maeneo mbalimbali kwa sasa mgonjwa aliyekuwa hapa anaweza kutibiwa na daktari aliyepo Mtwara kupitia mfumo wa tiba mtandao kwa njia ya video  ikiwa na kasi ya hali ya juu,”alisema.
Yahaya amesisitiza kuwa, maboresho hayo ya huduma za inteneti ndani ya TTTCL  yamelenga kuwezesha wateja kupata huduma kwa unafuu na uhakika hadi majumbani na kuwasiliana bila kikwazo ikiwemo kama vile kukatikatika kwa mawasiliano.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga akimtambulisha Bi. Janet Maeda Meneja Masoko wa Shirika la Mawasiliano Tanzania  kwa Dk. Peter Kisenge Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya KIKWETE (JKCI) wakati alipotembelea banda la Shirika hilo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa  katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

Dk. Peter Kisenge Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya KIKWETE JKCI  akipata maelezo kutoka kwa Mary Temba Afisa  kutoka Kitengo cha Wateja wakubwa TTCL  wakati alipotembelea banda la Shirika hilo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

Bi. Janet Maeda Meneja Masoko wa Shirika la Mawasiliano  Tanzania TTCL kushoto  akiwa na Ofisa Mawasiliano kutoka TTCL Bi Esther katika banada la TTCL.

Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL kutoka kitengo cha masoko wakiwa tayari kupokea wageni katika banda hilo.

Wageni mbalimbali wakipata huduma katika banda la TTCL viwanja vya sabasaba.

Judith Maruma ofisa Masoko wa Tpesa akizungumza na wageni waliotembelea katika banda hilo katikati ni Bw.Othman Abdulazak kutoka Shirikala THD Human Development akiwa na mkewe Mido Sharif.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirikala Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga akimkabidhi zawadi Dk. Peter Kisenge Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya KIKWETE (JKCI) mara baada ya kutembelea banda la Shirika hilo ili kujionea shughuli mbalimbali   katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirikala Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga akinzugumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Lughano Kusiluka wakati alipotembelea banda la Shirika hilo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo  katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Lughano Kusiluka akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea banda la Shirika hilo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo  katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Profesa Lughano Kusiluka akiondoka katika banda la Shirika la Mawiliano Tanzania TTCL huu akiwa ameongozana na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa chuo hico Bi. Rose Joseph mara baada ya kutembelea na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika hilo  katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa  Saba Saba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.