Tunapiga hatua kwa wale ambao ni wazalishaji wa mafuta ya kula nyumbani na wanapenda kuuza nje ya Nchi, tuko hatua chache kufikia kufunga maneno.
Jambo moja nalijua hakika, licha ya hali ya mafuta nyumbani kuwa katika hali iliyopo na nikirejea kutoka kikao tulifanya na wazalishaji wiki iliyopita, wako wazalishaji wenye mafuta na wanatafuta soko na hawajalipata na hapo ndipo kazi yetu ya Diplomasia ya Uchumi, Biashara, kuyalinda, kuyatetea, kuyapigania na kuyaendeleza Maslahi Mapana ya Tanzania inapokuja.
Je unamjua mzalishaji wa mafuta ya kula anayefanya ama “single au double refinery”? Mjuze anitafute haraka, tunafunga mlango, Alhamisi tarehe 22 Juni 2023.
Mzalishaji huyo anitafute kwa WhatsApp +5359333793.
Tunatengeneza fursa hii ili wazalishaji wa mafuta wapate faida yao ya haki na kutengeneza Ajira wa watu wetu na hasa vijana ili na wao wanunue alizeti kutoka kwa wakulima wetu, soko la uhakika tumelibaini katika Ukanda wa Karibe (Caribbean).
Usikae na fursa hii, kuwa Mzalendo Mjuze mhusika Haraka.
Balozi Polepole – Mkuu wa Kituo Havana