Mkurugenzi wa chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) Zanzibar Dkt.Mzuri Issa akizungumza na wakuu wa madawati ya kijinsia katika vyombo vya habari , na wahariri wa vyombo vya habari wakati walipokua katika mkutano maalum wa kuthibitisha na kutoa maoni kuhusiana na sera ya kijinsia kutumika katika vyombo vya habari huko Ofisi za TAMWA Tunguu Zanzibar.
Mkufunzi Chuo Kikuu cha Taifa Suza Imane Duwe akizungumza wakati alipokua akiwasilisha sera ya jinsia kwa wakuu wa madawati ya kijinsia katika vyombo vya habari na wahariri wa vyombo vya habari wakati walipokua katika mkutano maalum wa kuthibitisha na kutoa maoni kuhusiana na sera ya kijinsia kutumika katika vyombo vya habari huko Ofisi za TAMWA Tunguu Zanzibar.
Afisa habari mwandizi Baraza la Habari Tanzania MCT Shifaa Said Hassan akiongoza majadiliano wakati wa mkutano maalum wa kuthibitisha na kutoa maoni kuhusiana na sera ya kijinsia kutumika katika vyombo vya habari uliowashirikisha wakuu wa madawati ya kijinsia katika vyombo vya habari na wahariri wa vyombo vya habari huko Ofisi za TAMWA Tunguu Zanzibar.
Mkurugenzi idara ya habari maelezo Zanzibar Hassan Kahtib Hassan akichangia mada ya sera ya jinsia wakati wa mkutano maalum wa kuthibitisha na kutoa maoni kuhusiana na sera hiyo uliofanyika huko Ofisi za TAMWA Tunguu Zanzibar.
Afisa ufuatiliaji na tathmni Mohammed Khatibu akitolea ufafanuzi wa muitiko wa vyombo vya habari katika sera ya jinsia wakati wa mkutano maalum wa kuthibitisha na kutoa maoni kuhusiana na sera hiyo uliofanyika huko Ofisi za TAMWA Tunguu Zanzibar.Juni 07,2023.PICHA NA FAUZIA MUSSA -MAELEZO ZANZIBAR