Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati akifungua maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende,akielezea maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi.Sarah Mwaipopo ,akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akitoa salamu za mkoa wake wakati wa maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (hayupo pichani) wakati akifungua maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mercy Kiambe ambaye ni Mkurgenzi Msaidizi na Mdhibiti wa Ubora wakati alipotembelea banda la Wakili Mkuu wa Serikali katika Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyofanyika leo Juni 5,2023 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua Jarida Maalum la Miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili wa Serikali .Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt Boniface Luhende na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi.leo Juni 5,2023 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha Jarida Maalum la Miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali baada ya kulizindua kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 5, 2023. Wengine kutoka kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro, Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt boniface Luhende na kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea tuzo ya heshima kutoka kwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro ya kutambua mchango wake katika kuanzishwa kwa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kabla ya kuzungumza katika Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Juni 5, 2023. Katikati ni Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniface Luhende.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali yanayofanyika jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa,amezitaka taasisi zote za umma zenye mawakili wa serikali kuzingatia suala la utatuzi wa kero za wanachi ili kuepuka mrundikano wa mashauri ambayo hayana ulazima wa kuyafikisha Mahakamani.
Majaliwa, ameyasema hayo leo Juni 5,2023 jijini Dodoma wakati akifungua maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanazishwa kwa Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali na ufunguzi wa mafunzo kwa mawakili wa serikali.
“Mawakili wa serikali ongezeni bidii,juhudi weledi katika utendaji kazi wenu, fanyeni kazi kwa uzalendo kuweni wabunifu katika kuishauri serikali ipasavyo kuhusu mashauri yaliyopo na timizeni wajibu wenu”amesema Majaliwa
Aidha amesema kuwa ili kuhakikisha kuwa serikali inaendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi na kuendelea kujenga mazingira shindani ya kuvutia wawekezaji kwa ajili ya maendeleo Ofisi ya Wakili mkuu wa serikali kwa kushirikiana na Idara,wizara na taasisi za serikali zitumie kila fursa ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya majadiliano.
“Wizara, Idara na Taasisi za Serikali fanyeni kazi kwa karibu Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali katika uendeshaji wa mashauri ya madai na usuluhishi yanayohusu Serikali kwani ndiyo yenye mamlaka ya kisheria ya kusimamia mashauri yanayohusu Serikali na Taasisi zake ndani na nje ya nchi.“
Majaliwa amesisitiza kuwa nchi yetu bado inahitaji wawekezaji katika kuchangia kwa haraka ukuaji wa uchumi na kuongeza pato la taifa letu.
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema katika kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo ambayo inafanya kazi kwa weledi.
”Ofisi hiyo imeisadia serikali kuokoa kiasi cha Sh. trioni 7.57 kutoka na kumaliza mashauri yake kwa njia ya usuluhi.”amesema Dkt.Ndumbaro
Awali Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Boniphace Luhende amesema baada ya uzinduzi huo wanatarajia kuendesha mafunzo ya siku tatu kwa Mawakili wa Serikali zaidi ya 600 ili kuwaongezea ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Dkt.Luhende amesema tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo serikali imepata uwakilishi wa uhakika kwenye mashauri mblimbali ambayo yamekuwa yakifunguliwa dhidi yake na kwa gharama nafuu ndani na nje ya nchi.
“Katika kipindi cha miaka mitano hadi kufikia Mai 31, 2023 ofisi imeendesha jumla ya mashauri 7162 kati ya hayo mashauri 7025 ni ya madai na 137 ni ya usukuhushi katika mwaka wa fedha 2022/23 hadi Aprili mwaka huu Ofisi hii ilimaza mashauri ya madai 518 na kati yake 45 yaliisha kwa majadiliano na mashauri 15 ambapo kati ya hayo sita yalisha kwa majadiliano”amesema Dkt.Luhende