Na Victor Masangu,Kibaha
Mke wa mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Selina Koka ameahidi kupambana kwa ajili ya kuwaondoa wanawake katika wimbi la umasikini na kuwainua kiuchumi wanawake kuwapatia mitaji ya fedha katika kata zote 14 na kuwafungulia akaunti ili waweze kuanzisha biashara na kuondokana na kuwa tegemezi.
Selina ambaye pia ni mlezi wa UWT Wilaya ya Kibaha mji amesema ameyesema hayo wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa UWT katika kata mbili za Misugusugu na kongowe ambapo wamepatiwa fedha kwa ajili ya kufungulia akaunti na kuahidiwa kuingiziwa kiasi cha shilingi laki tano kwa kila kata ikiwa Kama mwanzo wa mtaji.
” lengo langu kubwa ni kuwasaidia wanawake wa UWT na wengune katika jimbo la kibaha na nimeshatoa fedha kwa ajili ya kufungulia akaunti katika kata tatu Hadi Sasa za mbwawa,misugusugu pamoja na kongowe na wakimaliza tu zoezi la kufungua nitawaingizia kiasi Cha laki tano kila kata,”alisema Mama Koka.
Alisema kwamba lengo lake kubwa ni kuona wanawake wanaunda vikundi vya ujasiriamali ambavyo pia ataviwezesha kuvipatia mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali katika kata hizo.
“Ninachotaka kukifanya ni kuwawezesha wanawake wajasiriamali ili waweze kuanzisha biashara zao ambazo zitawasaidia kujipatia fedha na kujikwamua kiuchumi na kwamba nitasaidia katika kata zote 14 za Jimbo hili,”alisema Mgonja.
Alifafanua zaidi Selina Koka aliongeza kuwa mikakati yake ni kuwafungulia akaunti wanawake wa UWT kwa kuwapa kiasi cha shilingi laki tano ili waweze kuanzisha biashara.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji Elina Mgonja amebainisha kwa kwa sasa katika kata ya misugusugu kumekuwa na maendeleo katika sekta mbali mbali.
Aliongeza kuwa Mbunge Koka amekuwa mstari wa mbele katika kusikiliza kero na changamoto mbali mbali zinazowakali na kuzifanyia kazi katika maeneo ya afya,elimu pamoja na miundombinu ya barabara.
“Kitu kitubwa sisi wanawake inabidi tuachane kabisa na mambo ya makando kando na kuwahimiza watu kulipa ada kwa wakati lengo ikiwa ni kujizatiti katika kuelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa,”alisema Mgonja.
Katika hatua nyingine alimpongeza kwa dhati mlezi wa UWT Selina Mgonja kwa juhudi zake za kusaidia wanawake katika kuwawezesha ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kwamba ziara yake ni kuangalia uhai wa chama.