Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja akizungumza Katika kikao kazi Cha Wahariri wa vyombo vya habari wanaofanya kazi Kwa karibu na Wizara hiyo Katika kikao kilichofanyika Hazina Ndogo ya Wizara ya Fedha jijini Arusha.
……………………………
Na Joseph Mahumi, Arusha
WIZARA ya Fedha na Mipango imesema inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa waandishi wa habari katika kuuhabarisha umma kusuhu Sera, Mipango, na Mikakati mbalimbali inayotekelezwa na serikali kupitia wizara hiyo.
Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Benny Mwaipaja, wakati akifungua semina elekezi kwa baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyolenga kuwajengea uelewa wa masuala mbalimbali yanayotekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango.
“Wananchi na umma wa watanzania kwa ujumla hawawezi kupata habari, Wizara inafanya nini, serikali inatekeleza nini bila ya ninyi na wadau wengine wa vyombo vya habari ambao hawako hapa.” Alifafanua Bw. Mwaipaja
“ Kama ambavyo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alivyoelekeza Wizara na Idara za Serikali kuwaambia wananchi mambo muhimu ambayo serikali inatekeleza, Sisi kama wizara tuna mambo mengi ya kuwaambia wananchi ikiwemo kuandaa Bajeti Kuu ya Serikali, namna tunavyotafuta rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo mmeiona ikiendelea kutekelezwa bila kukwama hii ni kwa sababu ya kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Fedha na Mipango.” Alisema Mwaipaja
Semina hiyo ni moja ya njia za kimkakati katika utekelezaji wa Mkakati wa Wizara wa Mawasiliano (Communication Strategy) ambapo Wizara inakutana na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari. Miongoni mwa mada zitakazowasilishwa ni utekelezaji wa Bajeti ya 2022/2023 na Mwelekeo wa Bajeti Kuu ya Serikali, Utekelezaji wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP),muongozo wa utoaji mafao na pensheni kwa wastaafu na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)
Baadhi ya wahariri Kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mawasilisho ya Mada Katika kikao kazi hicho.
Mtendaji Mkuu wa gazeti la Kilimo Bw. Kulwa Karedia akichangia mada Katika kikao kazi hicho kilichofanyika Ofisi za Hazina Ndogo ya Wizara ya Fedha jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Misa Tanzania na Mhariri wa Gazeti la Nipashe Bi. Salome Kitomari akiuliza swali Katika kikao kazi hicho.
Mhariri wa habari za Biashara na Uchumi Kutoka TBC Bi. Groria Michael akiuliza swali ili kupata Ufafanuzi wa baadhi ya mambo wakati kikao kazi hicho kikiendelea.
Mhasibu Mkuu Idara ya Pensheni, Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Eugenia M. Jairo akiwasilisha mada “Mwongozo wa Malipo ya Mafao ya Kustaafu”
Picha ya pamoja.