Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Julian Banzi akifungua semina ya kati ya BoT na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF inayofanyika Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam, watoa mada katika semina hii ni wataalamkutoka BoT watakao fafanua mambo mbalimbali kuhusu shughuliza benki kuu kama msimamizi mkuu wa sera ya fedha nchini Tanzania.
…………………………….
Naibu Gavana wa Benki Kuu Tanzania Julian Banzi amewataka wanahabari nchini kuwa mabalozi wakuieleza Jamii ielewe kuhusu Maendeleo ya Uchumi uliopo na sekta ya Fedha nchini.
Naibu Gavana BoT Banzi amesema hayo wakati akifungua semina ya Wahariri wa vyombo vya habari ambayo imefanyika BoT jijini Dar es salaam.
Banzi amesema kuwa kufanikisha kwa sekta hiyo ukuaji wake utasaidia kuimarisha benki kwa kuweza kukusanya rasilimali kwenda kwenye shughuli za kijamii.
“Ndugu wahariri tuneona tuwashirikishe ninyi Ili muweze kuelekeza ujumbe kwa wananchi kuhusu umuhimu wa sekta hii katika Masuala ya kiuchumi na Maendeleo ya nchi yetu”amesema Banzi
Aidha Banzi amewataka Wahariri Hao wa vyombo vya habari kufahamu kuwa ujuzi wanaoupata waendelee kuchangia mawazo yao ili kuimarisha na kulenga kutatua matatizo yanayojitokeza katika sekta hiyo.
Banzi ameendelea kusema kuwa ni vyema wakatumia fursa hiyo katika kuikumbusha Jamii namna wanavyopaswa kushiriki katika kufanya Maendeleo na hivyo kujiongezea kipato.
Naibu Gavana BOT amesema semina hiyo itakwenda kuwaimarisha uelewa wa namna ya kuandika taarifa zinazohusiana na benki hiyo lakini pia na uchumi kwa ujumla.
Noves Mosses Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT akikmaribisha Naibu Gavana wa BoT Bw. Julian Banzi hayupo pichani ili kufungua rasmi semina kati ya Benki hiyo na Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF inayofanyika leo katika benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Bw. Lwaga Mwambande Afisa Uhusiano Mkuu Mwandamizi idara ya Uhusiano akifafanua jambo wakati wataalam wakijibu maswali mbalimbali ya wahariri wa vyombo vya habari.
Bi Asimwe Bashagi Meneja Msaidizi Sera ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania akifafanua jambo wakati alipokuwa akijibu maswali ya wahariri wa vyombo vya habari katika semina iliyofanyika leo Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Jkuwaa la wahariri Tanzania TEF Bw. Bakari Machumu akitoa neno la shukuranikwa Benki Kuu ya Tanzania BoT kwa kuandaa semna hiyo kwa ajili ya kuwapa uelewa wahariri wa vyombo mbalimbali.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Bw. Julian Banzi akiwa ameketi katika semina hiyo pamoja na watoa mada wengine kutoka Benki Kuu ya tanzania.
Picha mbalimbali zikionesha waariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF wakifuatilia mada katika semina hiyo inayofanyika leo katika Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja.