Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu *Mhe. Dkt. Gwajima* ameshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake kuhusu Uongozi wenye kuleta Mabadiliko. Mkutano huo wa siku tatu unafanyika nchini Sudan Kusini. *Dkt. Gwajima* amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan*.
*************
Na WMJJWM, SUDANI YA KUSINI
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum *Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima* amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania *Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan* katika mkutano wa Kimataifa wa Wanawake kuhusu Uongozi wenye kuleta Mabadiliko, nchini Sudani ya Kusini.
Mkutano huo umefunguliwa leo Februari 13, 2023 na Rais wa Sudan Kusini *Mhe.Salva Kiir Mayardit* ambapo unaangazia masuala ya Wanawake na Uongozi.
Wadau zaidi ya 600 wa Kimataifa kutoka nchi 15 za Afrika wamehudhuria, wakiwemo Marais Wastaafu.
Kaulimbiu ya mkutano huo ni “Uongozi wa Mabadiliko kwa Wanawake, Amani na usalama”.