Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akipokea vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na Wajapan, kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9,2023 Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam.
***************************
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) wameendesha Kongamano la Ubunifu kwa Maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania ambalo litasaidia masuala ya ubunifu na uvumbuzi ili kusaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo sanjari na kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii.
Akizungumza katika Kongamano hilo leo Februari 9,2023 Jijini Dar es Salaam, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) – Taaluma, Prof. Boneventure Rutinwa amesema kipindi cha nyuma Chuo hicho hakikuwekeza vya kutosha kwenye masuala ya ubunifu na uvumbuzi ili kusaidia nchi kupiga hatua kimaendeleo sanjari na kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii.
“Kwasasa tunashirikiana na Sekta husika za masuala haya ya ubunifu na uvumbuzi ili kuhakikisha changamoto mbalimbali katika jamii zinatatuliwa na nchi kwa ujumla inapiga hatua kimaendeleo”. Amesema
Amesema mashirikiano yaliyopo sasa kati ya Tanzania na Japan, kongamano hilo linajadili uanzishwaji wa ‘programu’ ya mafunzo ambayo yataiwezesha Tanzania kupitia UDSM kujifunza kutoka kwa Japan na kupata uzoefu wao kama taifa lililoendelea bila kuiga na kufuata mbinu za Mataifa ya Magharibi.
Prof. Rutinwa amesema: “Ushirikiano huu wa nchi yetu Tanzania (UDSM) na Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) sio kwenye teknolojia ya viwanda pekee, hata kwenye Sayansi ya Jamii katika lengo la kutatua matatizo na changamoto kwa jamii ya Watanzania na nchi kupiga hatua kimaendeleo.”
Prof. Rutinwa amesema kuwa awali kulikosekana mashirikiano mazuri baina ya Sekta husika (Industry Academia Linkages) ambazo tayari zimeendelea ili Tanzania kupitia Chuo hicho kujifunza na kusaidiana katika kubadilisha uzoefu wa masuala hayo ya maendeleo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael alisema midahalo kwenye Kongamano hilo yaliangazia masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kutokana na mabadiliko yake, Serikali ya Tanzania imeweka nguvu zaidi katika masuala hayo kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu.
“Serikali inazingatia sana masuala ya TEHAMA katika kujenga ubunifu wa Watanzania, ndio maana Serikali tumeona kuna umuhimu kuanza kufundishwa kuanzia Shule za Msingi hadi Vyuo Vikuu, hivyo hivyo lazima kuwa na muendelezo kulingana na matekwa ya dunia,” amesema Dkt. Francis
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akizungumza katika Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9,2023 Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akizungumza katika Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9,2023 Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akizungumza katika Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9,2023 Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) – Taaluma, Prof. Boneventure Rutinwa akizungumza katika Kongamano la ubunifu kwa maendeleo ya nchi za Japan na Tanzania lililofanyika leo Februari 9,2023 Chuo Kikuu cha Cha Dar es Salaam (UDSM) Jijini Dar es Salaam.