Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Eng. Peter Ulanga akibadilishana hati za mkaaba wa makubaliano na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jamhuriya Kidemokrasia ya Congo (SCPT) Papy Ethiere Nkire mara baada ya kusainiana makubaliano ya kupeleka Mkongo wa Mwasiliano nchini humo, hafla hiyo imefanyika makao makuu ya shirika la Mawasiliano TTCL mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo
……………………………………………………..
KATIKA kuendelea kutimiza majukumu ya kuimarisha usalama, ufanisi wa kiuchumi na biashara Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) limesaini makubaliano yasiyo ya kutoa taarifa (Non disclosure Agreement,) na Shirika la Posta na Mawasiliano la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia mradi wa kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutoka Kigoma, Tanzania kwenda Kalame, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano hayo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Eng. Peter Ulanga amesema Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kutoka Kigoma, Tanzania hadi Kalame kupitia Ziwa Tanganyika unatarajiwa kuwa wa kilometa 150 hadi 160 na makubaliano hayo baina ya Nchi hizo mbili ni katika kushirikiana na kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa ufanisi.
” Mradi huu ni muhimu sana kwa Nchi zetu kwani utafungua njia za mawasiliano kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na Nchi jirani za Kenya, Uganda, Malawi, Msumbiji na nje ya Bara la Afrika… Pia mradi utaiwezesha Tanzania kufika katika nchi za Pwani ya Magharibi kupitia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.” Amesema.
Aidha amelihakikishia Shirika la Posta na Mawasiliano la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwa, Tanzania ni moja kati ya Nchi mbili Afrika zenye uwezo wa kuunganisha bahari ya Hindi na Bahari ya Atlantiki kwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
” Tunayo miundombinu madhubuti ya mawasiliano na Serikali makini na wezeshi hivyo matarajio yetu kuwa mradi huu utafanikiwa kwa kiasi kikubwa.” Amesema.
Aidha ameishukuru Serikali kupitia Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye kwa miongozo, Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana katika mradi huo pamoja na ujumbe wa Shirika la Posta na Mawasiliano la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwasili Tanzania na kusaini makubaliano hayo muhimu yatakayowezesha kukamilisha mradi huo mkubwa wa kujenga miundombinu ya mawasiliano kwa maslahi ya Nchi hizo mbili.
Akizungumza kwa niaba ya Postamasta mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Costastine Kasese ameishukuru TTCL kwa kushirikiana katika makubaliano hayo na ugeni huo ambao umetembelea maeneo mbalimbali yenye fursa la kibiashara.
Amesema makubaliano hayo yatasaidia katika mawasiliano ya simu, intaneti pamoja na huduma za Posta na kueleza kuwa Shirika la Posta litashirikiana na DRC katika maeneo matatu muhimu ya biashara za mipaka, biashara mtandao pamoja na ubadilishanaji wa teknolojia na utoaji wa huduma za mawasiliano kwa njia ya Posta.
Kwa upande wake kiongozi wa msafara huo ambaye Waziri mshauri wa Mkuu wa Wizara ya Posta na Mawasiliano na TEHAMA (DRC,) Azitemina Fundji Blaise ameeleza kuwa, Kongo na Tanzania wamekuwa na mahusiano mazuri na Balozi za nchi hizo zimekuwa zikionesha juhudi ya kuboresha mahusiano hayo.
Amesema ushirikiano huo utaboresha na kunufaisha wananchi kupitia huduma za mawasiliano kupitia TTCL, Shirika la Posta na Mawasiliano la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Shirika la Posta Tanzania.
Blaise amezihakikishia Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutufaika na mradi huo kiuchumi pamoja na biashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Eng. Peter Ulanga na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (SCPT) Papy Ethiere Nkire waionesha hati za mkataba mara baada ya kusainiana makubaliano ya kupeleka Mkongo wa Mwasiliano nchini humo. hafla hiyo imefanyika makao makuu ya shirika la Mawasiliano TTCL mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Eng. Peter Ulanga na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (SCPT) Papy Ethiere Nkire wakisaini hati za mkataba mkataba wa makubaliano ya kupeleka Mkongo wa Mwasiliano nchini humo, hafla hiyo imefanyika makao makuu ya shirika la Mawasiliano TTCL mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL,) Eng. Peter Ulanga akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika makao makuu ya shirika la Mawasiliano TTCL mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo, hafla hiyo imefanyika makao makuu ya shirika la Mawasiliano TTCL mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya pamoja.