Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa akisaini Mkataba na wakandarasi kwaajili ya ujenzi wa majengo matano ya Chuo hicho, hafla ambayo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa akisaini Mkataba na wakandarasi kwaajili ya ujenzi wa majengo matano ya Chuo hicho, hafla ambayo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Elimu) Prof. Carolyne Nombo akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya NIT na wakandarasi ambao watajenga majengo matano ya Chuo hicho, hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kheri James akizungumza akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya NIT na wakandarasi ambao watajenga majengo matano ya Chuo hicho, hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zacharia Mganilwa akizungumza katika hafla ya utiaji saini kati ya NIT na wakandarasi ambao watajenga majengo matano ya Chuo hicho, hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam
**********
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeingia mkataba na wakandarasi kujenga majengo matano ya Chuo hicho ambao ni sehemu ya mradi wenye thamani ya Bilioni 49 na unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Oktoba 28,2022 Jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Elimu) Prof. Carolyne Nombo amesema Serikali itasimamia mradi huo mpaka kuhakikisha malengo yanafikiwa.
“Kwa wakandarasi ninawaomba mfanye kazi kwa bidii na uweledi ili kuhakikisha kuwa mradi unakamilika kwa muda uliopangwa yaani miezi 12.” Amesema Prof.Nombo.
Aidha amewataka wakandarasi hao kujenga majengo bora kulingana na thamani yake pia kukabidhi majengo hayo kwa muda wa makubaliano kwenye mkataba.
Amesema majengo hayo ni muhimu kwa ustawi wa mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji na kuomba ujenzi uanze kwa kasi huku wakizingatia taratibu zote za kisheria na za kiufundi ili kukamilisha kazi hiyo kwa ubora na kwa muda mfupi inavyotarajiwa”
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Zacharia Mganilwa amesema mkataba wa ujenzi uliosainiwa unathamani ya shilingi Bilioni 21 ambapo ujenzi huo huo utafanywa kwa mwaka mmoja.
Amesema chuo hicho kimeanzisha kituo cha umahiri katika taaluma ya anga na masuala yote ya usafirishaji ambapo tayari NIT imefika asilimia 75 ya utekelezaji.