Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) umewahimiza
waajiri kuchangamkia fursa ya punguzo la michango lililotolewa na Serikali ya
Awamu ya Sita kuanzia Julai Mosi 2021 ili kulinda nguvu kazi na kuongeza ari ya
wafanyakazi wao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi Dkt. John Mduma wakati akizungumza na wahariri baada ya
Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), 2022 uliofanyika
Unguja, Zanzibar.
Dkt. Mduma amesema katika mafanikio ya siku
365 za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, WCF inajivunia kuboresha mazingira ya
uwekezaji na biashara nchini kwa kukubaliwa kutoa punguzo la uchangiaji kutoka
1% kwa waajiri wa sekta binafsi hadi kufikia asilimia 0.6% na punguzo la riba
(interest) la madeni ya nyuma ya michango kwa sekta zote kutoka asilimia 10%
mpaka asilimia 2%.
Dkt. John Mduma amefafanua kuwa, moja ya
wajibu wa WCF ni kulinda nguvu kazi ya wafanyakazi kuanzia matibabu ya
Mfanyakazi aliyepata ajali au ugonjwa kutokana na kazi ili kuwawezesha Waajiri kuendelea
kusimamia uzalishaji wakati wafanyakazi wao wakiendelea kuhudumiwa na WCF.
“Nakushukuru sana Mwenyekiti wa TEF kwa kutupa
nafasi hii ya kuweza kushiriki kwenye hadhira hii ambayo kimsingi inatuwezesha kuufahamisha
Umma kuhusu WCF inavyowajibika katika kulinda nguvu kazi ya Tanzania. Tunapenda
kuwahimiza Waajiri wa Sekta Binafsi kuchangamkia fursa hizi za uboreshaji
ikiwemo punguzo la uchangiaji na tozo ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima
kati yao na wafanyakazi” Alisema Dkt. Mduma.
Dkt. Mduma pia alibainisha kuwa WCF
inashirikiana kwa karibu na Taasisi ya Hifadhi ya Jamii Zanzibar, ZSSF ikiwemo kubadilishana
mawazo na kupeana uzoefu juu ya masuala ya Fidia kwa Wafanyakazi.
“Sisi kama wabobezi karibu miaka saba sasa ya
utekelezaji wa Sheria ya Malipo ya Fidia kwa Wafanyakazi, tumekuwa tukipeana
uzoefu na kujadiliana nao ili nao waweze kuelekea kwenye upande huo.”
Naye Mtaalamu wa Takwimu kutoka WCF, Bw. James
Tenga aliwajulisha wahariri kuhusu masuala mbalimbali ya utekelezaji wa
majukumu ya Mfuko huo ikiwa ni pamoja na taratibu za madai ya fidia kwa Mfanyakazi
anapoumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi ili aweze kulipwa fidia.
Amesisitiza pia umuhimu wa Mwajiri kujisajili
katika Mfuko na kuwasilisha michango ya kila mwezi ambapo kwa sasa huduma zote
za Mfuko huo hutolewa kwa njia ya mtandao ikiwemo uwasilishaji wa madai.
Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF), 2022 umefunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Unguja, Zanzibar na unaongozwa na kauli mbiu
isemayo “Uchumi wa Buluu na Mawasiliano ya Umma”.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (kushoto)
akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John
Mduma, cheti cha shukrani kutokana na Mfuko huo kuwa miongoni mwa Taasisi zilizodhamini Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) unaofanyika mjini Unguja,
Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwenye ukumbi wa
Idrisa Abdulwakil, kisiwani Unguja, Zanzibar Machi 9, 2022.
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akihutubia
wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwenye ukumbi wa
Idrisa Abdulwakil, kisiwani Unguja, Zanzibar Machi 9, 2022
wa Habari na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Mhe. Nape Nnauye, akizungumza
kwenye mkutano huo.
wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Tabia Maulid Mwita, akizungumza
kwenye mkutano huo.Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu ya Zanzibar, Bw. Charles Hillary.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi (katikati) na viongozi waliokuwa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa Mkutano huo.