Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akiambatana na Msemaji Mkuu wa Serikali,Dkt.Hassan Abbasi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA-Zambia, Mhandisi.Bruno Chingandu (wa kwanza kulia) na Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah wa pili kulia wakiwa katika uzinduzi wa mitambo ya kunyanyulia mizigo stesheni ya Fuga.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye(wa pili kutoka kushoto) akivaa kofia kujiandaa kuwasha moja ya mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa Umeme JN HPP iliyopo katika Stesheni ya Fuga, wa kwanza kushoto ni Meneja wa TAZARA ,Mkoa wa Tanzania, Fuadi Abdallah.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akiendesha moja ya mitambo ya Kunyanyulia mizigo iliyoko katika stesheni ya Fuga wakati wa ufunguzi wa mitambo hiyo hapo jana Agosti 19, 2019.
Wafanyakazi wa Stesheni ya Fuga wakishuhudia uwezo wa mtambo aina ya Raech Stacker wa kunyanyua mizigo mizito katika stesheni ya Fuga uliozinduliwa jana na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akitelemka kutoka kwenye moja ya mtambo wa kunyanyulia mizigo mara maada ya kuuzindua hapo jana katika Stesheni ya Fuga itayotumika kopokea na kusafirisha mizigo kwenda mradi wa Umeme JN HPP.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akipata maelezo fulani kutoka kwa Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi wakati wa uzinduzi wa mitambo ya kunyanyulia mizigo ya ujenzi wa mradi wa umeme JN HPP uliofanyika katika Stesheni ya Fuga.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Atashasta Nditiye, akipata maelezo fulani kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya usambazazi mitambo ya kunyanyulia mizigo ya Eristic (t) Investment Company, Hassan Kipussi katika uzinduzi wa mitambo hiyo uliofanyika katika Stesheni ya Fuga jana Agosti 19, 2019.
(Picha na Idara ya Habari-MAELEZO)
**************
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe.Atashasta Nditiye
amazindua Rasmi Vifaa vya Kunyanyulia Makontena ya Mizigo na Vifaa vizito vya
utekelezaji wa ujenzi wa Mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere Hydro Power
Project (JN HPP).
Akizungumza jana katika stesheni ya fuga, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali
imenunua vifaa hivyo ambavyo ni Reach Stacker 2 zenye uwezo wa kunyanyua tani
45, Mobile crane yenye uwezo wa tani 15 na Forklift 2 zenye uwezo wa tani 5 na
zimegharimu Tzs Bilioni 3.5.
“Vifaa hivi vimenunuliwa na Serikali ili kuiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu
iliyopewa ya upokeaji makontena ya mizigo mizito ya ujenzi wa bwawa la kufua
umeme la JN HPP, katika mto Rufiji, mradi utakozalisha Megawati 2,115 na
kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda”, Naibu Waziri Nditiye.
Aidha, Waziri Nditiye alisema kuwa Serikali itaendelea kuishika mkono TAZARA ili
kuhakikisha inafanya kazi ufanisi mkubwa kwenye utekelezaji wa mradi wa kufua
umeme JN HPP na ndiyo maana imetoa Tsh. Bilioni 10 ili kununua Traction Motors
42 kwa ajili ya vichwa saba vya treni za masafa marefu na sogeza ambazo zitaanza kuwasili mwezi oktaoba.
Waziri Nditiye aliongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inawahakikishia wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia
(TAZARA)kuwa itaendelea kulipa mishahara yote kwa kipindi chote cha mwaka wa fedha 2019/2020 na tayari imetanga kiasi cha shilingi bilioni 14.9 zimetengwa.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia
(TAZARA) alisema kuwa ni jambo kubwa na heshima kwa Mamlaka hiyo kupewa
majukumu ya kupoea mizigo ya utekelezaji wa ujenzi wa Mradi wa Umeme JN HPP.
“Napenda kusema kuwa Serikali ya Tanzania, Chini ya Rais Dkt.John Pombe
Magufuli, ilituamini na kutupatia kiasi cha Shilingi Bilioni tano ili kukarabati
stesheni ya Fuga kwa kujenga Stendi ya kupokea na kusafirisha mizigo, kununua
vifaa vitakavyosaidia kunyanyua mizigo hiyo kwa ufanisi mkubwa”, Mhandisi. Bruno Chingandu.
Mhandisi Chingandu alisema kuwa vifaa hivyo viyakuwa na uwezo mkubwa wa
kutosheleza mahitaji ya kupokea mizigo ya ujenzi wa mradi mkubwa wa kihistoria
wa kufua umeme wa JN HPP, kwani tani kati ya 5 mpaka 45 zitanayanyuliwa na
vifaa hivyo.
Aidha, Mhandisi Chingandu alisema kuwa Serikali imetekeleza kwa vitendo ununuzi
wa Traction motor 42 kwa ajili ya treni ya masafa marefu kwa kutoa Tsh.Bilioni 10, hivyo itaiwezesha TAZARA kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na
kuliwezesha Shirika hili kurejera tena katika utendaji mkubwa.
Naye Meneja wa TAZARA Mkoa wa Tanzania, Fuad Abbdalah, alisema kwamba
Serikali imewapatia Fedha za ujenzi na ununuzi wa vifaa ni heshima kubwa kwa
Shirika hilo kwani limeingia kwenye historia ya mageuzi ya Serikali ya Awamu ya
Tano.
“Leo tunashuhudia kitendo kikubwa cha kuzindua hizi mashine tano za kunyanyulia mizigo mizito ya ujenzi wa Mradi wa kihistoria wa JN HPP, Mashine hizi zina uwezo mkubwa wa kunyanyua Tani 5 mpaka 45, uwezo stahiki kabisa kuhudumia mizigo yote inayohitajika kwenye mradi wa umeme mto Rufiji”; Fuad Abbdalah, Meneja TAZARA mkoa wa Tanzania.
Fuad aliongeza kuwa Serikali imeliamini Shirika hilo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano ameahidi kurudisha uafanisi wa utendaji wake na katika ziara yake ya
kwenda kuzindua Mradi wa umeme JN HPP alisema atahakikisha anashirikiana na
Rais wa Zambia ili kurudisha heshima ya TAZARA.
Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt.Hassan Abbasi alisema Serikali
imetekeza ukarabati wa stesheni ya kupokea na kushushia mizigo ya Fuga
itayosaidia ujenzi wa Mradi wa Umeme wa JN HPP kufanikiwa kwa haraka Zaidi.
“Tunatekeleza Uboreshaji huu wa Stesheni ya Fuga, tumeleta mitambo ya kisasa
mikubwa kabisa ambayo imedhaminiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa ajili ya kuhudumia ujenzi wa bwawa la kufua umeme JN HPP, kwa
hiyo mitambo hii imefika, inafanya kazi na inasambazwa na Kampuni ya kizawa”,
Dkt.Abbasi.