PROFESA Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam UDSM Fiken Senkoro akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo leo |
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo wakiwa kwenye mkutano huo
Umakini ukiendelea kwenye kikao hicho |
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
BARAZA la Kiswahili la Taifa Tanzania (Bakita) limesema kwamba vitendo vya uendeshaji vituo vya kufundisha Kiswahili kwa wageni nchini ambavyo havijasajiliwa na Serikali ni kinyume cha sheria na kanuni za baraza hilo hivyo hawatasita kuvichukulia hatua ikiwemo kuvifungia.
Hayo yalisemwa leo na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahi Tanzania (Bakita) Consolata Mushi wakati wa mkutano wa Bakita na wadau wa vituo vinavyofundisha Kiswahili kwa Wageni nchini uliofanyika mjini Tanga.
Mkutano huo unatokana wa kwanza unajumuisha wamiliki wa vituo na wadau wa vituo vya Kiswahili kwa wageni unatokana na kanuni na sheria za Bakita.
Alisema Tanzania kuna vituo 15 vya kufundisha Kiswahili lakini wanajua vipo zaidi ya hivyo hivyo wanapaswa kutambua kwamba kama wataendesha mafunzo bila kusajiliwa na baraza ni kosa hivyo hawatasita kufungia kituo hicho.
Alisema wao kama Baraza hawataki kufika huko ndio maana wanatoa wito wakutane wajadili na kusajili vituo kutokana na kwamba wanaposema wanadhibiti ufundishaji wa kuswahili Tanzania ni kuhakikisha walimu wanaotumiwa kufundisha lugha ya Kiswahili wanauwezo wa kufundisha.
Alisema pia wawe na uhakika wa kufundisha na kila mtu kama alivyobainisha hapo mwanzoni huku akisisitiza kwa kutumia fursa hiyo kuwataka watu wenye vituo vya kufundisha Kiswahili na havijasaliwa waende baraza la kiswahii wakasajiliwe vituo vyao.
“Na sio kwamba tunasema waende wakajisajili ni kwa mujibu wa kanuni na sheria za baraza hilo kwani sababu huwezi kufanya jambo ilihali utambuliki na baraza na kwani bakita ni chombo cha sheria hivyo ukisajiliwa huko unatambuliwa na serikali kama mtu ambayo unakituo ambacho kinatoa mafunzo ya Kiswahili Tanzania “Alisema Kaimu Katibu huyo.
Alisema kwamba wanaona Kiswahili kinapiga hatua kubwa ambazo si za kawaida waswahili wanasema kimepiga kunako siku maalumu kila mwaka 7, Julai imethibitishwa na Shirika la Unesco kunamaanisha kiswahil kwa sasa ni lugha inayoheshimika duniani imebeba dhamana kubwa.
“Kiswahili kimebeba dhamana kubwa kama unavyojua kulikuwa na dhamana kubwa ya lugha sita zilizokuwa zimetengewa siku maalumu dunia Kingereza, kichina, kifarasa, kiarabu, kispaniol, kiroshia”Alisema Kaimu Katibu huyo.
Awali akizungumza katika mkutano huo kutoka Shirika la Urithi wa Utamaduni wa Kiswahili (SUUKI) Tanga Mwalimu Ramadhani Kasimu alisema mkutano huo wa wadau wote wanaofundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni na wao washiriki wenyeji ni muhimu sana kwao kutokana na kwamba sasa kiswahili ni tunu iliyopewa heshima kubwa sio Tanzania bali mpaka nje ya nchi.
Hata hivyo aliishauri jamii jamii kwa sababu kimeshakuwa tunu wakitumie Kiswahili kwao kwenye Nyanja mbalimbali kiwape manufaa yenye tija na wakithamini ili kiweza kuwasaidia.