*********************
Na Mwamvua Mwinyi, Mkuranga
Bodi ya nyama Tanzania inaendelea kutoa elimu kwa wafugaji katika halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Lengo ni kuongeza tija kwa wafugaji sambamba kusaidia kupunguza migogoro ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi kwa kuwapa elimu.
Pia kuhimiza ufugaji wa kisasa na kuondokana na ufugaji wa makundi ya mifugo ya ng’ombe holela hali inayosababisha kulisha katika mazao ya wakulima.