Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya(wa tatu kushoto kwa waliokaa), akiwa katika picha ya Pamoja na Wakurugenzi  wa Sekta ya Uchukuzi na wadau  waliohudhuria Mkutano wa 14 wa Mapitio ya upimaji utendaji kazi wa sekta ya Uchukuzi (JTSR-2021) katika Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Washiriki  wa Mkutano wa 14 wa  Mashauriano ya Wadau wa sekta ya Uchukuzi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi , Mhandisi Godfrey kasekenya(hayupo pichani) wakati wa akifungua  mkutano huo, Jijini Dar es salam.

Mkurugenzi wa Sera na Mipango  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Aunyisa Meena ,akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa 14 wa mapitio ya Utendaji kazi wa Sekta ya Uchukuzi(JSTR 2021), katika Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akikagua baadhi ya mabanda yaliyoshiriki  kwenye Mkutano wa 14 wa mapitio ya Utendaji  kazi  wa Sekta ya Uchukuzi(JSTR 2021), katika Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akihutubia Mkutano wa 14 wa mapitio ya Utendaji  kazi wa Sekta ya Uchukuzi(JSTR 2021), katika  ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.