mjini Jesca Msambatavangu akiwa na viongozi wa duka la Dar Ceramica Center wakiwa wameshika cheti nafuraha kubwa ya ufunguzi wa duka hilo.
mjini Jesca Msambatavangu ubora wa vifaa vya ujenzi vinavyopatokana katika duka hilo.
Balozi wa maduka ya Dar Ceramica Center Irene Paul akiteta jambo mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavanguna
Shule ya Msingi
Wilolesi Mkoani Iringa Imepokea msaada wa masinki 15 ya vyoo kutoka Duka la
vifaa vya Ujenzi la Dar Ceramica Centre lililopo Manispaa ya Iringa msaada
ulilenga kupunguza tatizo la uchakavu wa vyoo katika shule hiyo na kuwaondosha
wanafunzi katika hatari ya kukabiliwa na magonjwa mbalimbali yatokanayo na
ukosefu wa vyoo bora
Akizungumza wakati
wa uzinduzi wa duka la Dar Ceranica Centre lililopo katika manispaa ya
Iringa,meneja mauzo wa kanda ya kusini John Gondwe alisema kuwa wamefungua tuka
hilo kwa lengo la kuwafikishia huduma ya vifaa bora vya ujenzi wakazi wa mikoa
ya nyanda za juu kusini.
Alisema kuwa wanauzoefu wa kuuza vifaa hivyo bora
zaidi nchini kwa zaidi ya miaka 25 ambapo wamefanikiwa kufungua jumla ya maduka
11 ambayo yanauza vifaa vya ujenzi hapa nchini Tanzania.
Gondwe alisema
kuwa wameamua kutoa msaada wa masinki 15 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule
ya msingi Wilolesi baada ya kugundua kuwa shule hiyo ina vyoo chakavu ambavyo
sio rafiki kwa matumizi ya wanafunzi wa shule hiyo.
Alisema kuwa
duka hilo limekufunguliwa mkoani Iringa kwa lengo la kuwarahisishia wananchi
kupata vifaa bora ya ujenzi ambavyo kwa asilimia kubwa vinatoka nje ya nchi.
Gondwe alisema
kuwa wanavifaa bora na Imara vya ujenzi kama vile tiles kutoka Hispania,bomba,miksa,beseni,bathtubs
na Jacuzzi kutoka nchini Ureno,mashine za kuchemshia maji ya moto vyooni au
bafuni kutoka katika nchi ya Itali na vifaa vyote vinavyonunuliwa katika duka
hilo vinakuwa na warranty ya uhakika.
Alisema kuwa
duka hilo limekuja na neema kwa mafundi ujenzi wa mkoa wa iringa na nje ya mkoa
wa Iringa kwa kuwa uongozi wa duka hilo umeamua kuwapatia elimu ya kuongea
ujuzi wa ufundi wao.
Aidha Gondwe
alisema kuwa fundi Lazaro Mwinuka ameibuka mshindi wa shindano la Serereka na
Dar Ceramica wa mkoani Iringa kwa kupata zawadi ya vifaa vyote vya ujenzi
ambavyo vitamsaidia kuongeza ufanisi wa kazi zake.
Gondwe alimalizia
kwa kuwaomba wananchi wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa kwenda kununua
vifaa bora na Imara kutoka katika duka la Dar Ceramica Center ambalo lipo
katika jengo la Hanspoppe mkabala na hotel ya M.R.
Kwa upande wake
mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini Jesca Msambatavangu
alisema kuwa wananchi wa mkoa wa Iringa wamebahatika kupata duka ambalo linauza
vifaa bora na imara vya ujenzi mkoani humo.
Alisema kuwa
amefanikiwa kuviona vifaa hivyo ambavyo vinauzwa kwenye duka hilo kuwa ni vifaa
vyenye ubora na imara kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali kwa gharama
nafuu kabisa.
Msambatavangu alisema
kuwa kufunguliwa kwa duka hilo kunaongeza ajira kwa wananchi wa jimbo la Iringa
Mjini na maeneo ya jirani kwa kuwa mafundi wote watakuwa wanapata kazi nyingi
kwa kuwa wanakuwa wanatumia vifaa bora na imara kutoka katika duka la Dar
Ceramica Center lililopo manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa
faida nyingine ambayo inapatika kwa uwepo wa duka hilo ni kuinua kiwango cha
uchumi kwa kushirikiana na jamii ambayo ndio watakuwa wateja na watumizi wa
vifaa hivyo.
Msambavangu alisema
kuwa amejitolea kuwa balozi wa duka hilo na kuwaomba wananchi wengine kujitolea
kulitangaza duka hilo lenye vifaa bora na imara vya ujenzi kwa wananchi wote wa
mkoa wa Iringa na nje ya Iringa.
Naye balozi wa
maduka ya Dar Ceramic Center,Irene Paul aliwataka wakazi wa mkoa wa Iringa
kununua vifaa bora na imara vya ujenzi katika duka hilo ambalo limefunguliwa
katika manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa
kufunguliwa kwa duka hilo kunaleta fursa kwa wananchi wa mkoa wa Iringa kwa
kuweza kununua vifaa vya ujenzi vilivyo bora na imara kwa gharama nafuu na
vyenye warranty ya uhakika.