Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Shadrack Makubi,akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 9,2021 jijini Dodoma kuelekea Oktoba 10 ambayo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani.
DAKTARI Bingwa wa Magonjwa ya akili katika Hospitali ya Taifa ya magonjwa ya Akili Mirembe Dkt.Innocent Mwombeki,,akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 9,2021 jijini Dodoma kuelekea Oktoba 10 ambayo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili Mirembe,Dkt.Paul Lawale,akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 9,2021 jijini Dodoma kuelekea Oktoba 10 ambayo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifatilia hotuba wakati wa taarifa kuelekea Oktoba 10 ambayo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani
………………………………………………………………………..
Na Erick Mungele,Dodoma
KUELEKEA kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya akili Duniani na maadhimisho mapambano dhidi ya matumizi ya pombe zaidi ya watanzania milioni 7 wana matatizo ya afya ya akili huku Mkoa wa Dar es salaam ukitajwa kuwa kinara kwa kuwa na watu wengi wenye tatizo hilo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 9.2021,Jijini Dodoma ,Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyoyakuambukiza kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Shadrack Makubi kuelekea Oktoba 10 ambayo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya Afya ya Akili Duniani,amesema kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha watanzania milioni saba wana matatizo ya afya ya akili.
”Mkoa wa Dar es salaam ni kinara kwa kuwa na watu wengi wenye matatizo ya afya ya akili kutokana na watu wengi matatizo hayo kwenda Jijini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.”amesema Bw.Makubi
Aidha watu zaidi ya milioni 300 wana matatizo ya afya ya akili duniani.
Kwa upande wake,Daktari Bingwa wa Magonjwa ya akili katika Hospitali ya Taifa ya magonjwa ya Akili Mirembe Dkt.Innocent Mwombeki amewaasa akina mama kuacha matumizi ya vilevi wanapokuwa wajawazito ili kuwanusuru watoto walio tumboni kuzaliwa wakiwa na matatizo ya afya ya akili.
“Mama mjamzito kutumia vilevi inasababisha ukuaji wa ubongo wa mtoto kuathirika na kusababisha mtoto kuzaliwa na matatizo ya afya ya akili na kuendelea kuongeza idadi ya wagonjwa wenye matatizo ya afya ya akiliu.ämesema Dkt.Mwombeki
Vile vile ametaja sababu nyingine inayosababisha matatizo ya afya ya akili ni pamoja na mtoto kutolishwa vizuri tangu anapozaliwa,kufanyiwa ukatili mbalimbali ,vipigo kwa watoto na manyanyaso mbalimbali.
Amewasihi akina mama wajawazito kuacha kutumia vilevi ili kunusuru afya za viumbe vilivyo kwenye matumbo yao.
“Kuna magonjwa ya akili yapo ndani kwa ndani kama Sonona na wasiwasi hili la vinasaba linatoka katika ukoo na mtu wa namna hii akitumia kilevi mfano Bangi anaripuka moja kwa moja,”amesema Dkt.Mwombeki
Awali Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya afya ya akili Mirembe,Dkt.Paul Lawale amesema wanakabiliwa na changamoto ya miundombinu ya hospitali hiyo kuwa chakavu kutokana na kujengwa wakati wa mkoloni miaka 95 iliyopita.
Amesema Hospitali hiyo inahitaji uwekezaji zaidi kwani kwa sasa wanauwezo wa kuhudumia wagonjwa 590 wakati waliopo kwa sasa ni 400
“Pia tuna changamoto ya kuwarejesha katika jamii wagonjwa wanapopata nafuu,tunajua wanatoka Mikoa mbalimbali sasa wanapopata nafuu ndugu huwa hawaonekani hivyo tunakutana na wakati mgumu,”amesema Dkt.Lawale