Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta kuelekea Siku ya Posta Duniani katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta kuelekea Siku ya Posta Duniani katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta kuelekea Siku ya Posta Duniani katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akizungumza wakati uzinduzi rasmi wa Duka Mtandao la Posta ulioambatana na Maadhimisho ya Wiki ya Posta kuelekea Siku ya Posta Duniani katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma

Kaimu Posta Masta Mkuu, Macrice Mbodo,akizungumza wakati wa uzinduzi wa  duka la Posta Mtandaoni (Posta Online Shop) ambapo umeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Posta Duniani,yalianza leo Oktobar 6,2021 hadi 9,2021 jijini Dodoma.

NAIBU Waziri Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi.Andrea Kundo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada kuzindua  duka la Posta Mtandaoni (Posta Online Shop) ambapo umeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Posta Duniani,yalianza leo Oktobar 6,2021 hadi 9,2021 jijini Dodoma.

………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

NAIBU Waziri Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Mhandisi. Andrea Kundo  amezindua duka la Posta Mtandaoni (Posta Online Shop) ambalo litawawezesha wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kununua na kuuza bidhaa zao kwa njia ya mtandao huku  akilitaka  Shirika la Posta kujipanga kuteka  soko la biashara Mtandaoni kwani wanamatawi  350 nchini.

Akizungumza leo,Oktoba 6,2021 jijini Dodoma  wakati wa uzinduzi wa duka hilo ambao umeenda sambamba na maadhimisho ya siku ya Posta Duniani,Mhandisi Kundo amewaomba watanzania kutumia huduma za Shirika hilo kwani kwa sasa zimeboreshwa kwa kiasi kikubwa.

Mhandisi Kundo amesema Shirika hilo ndilo lenye mtandao mkubwa hivyo wanatakiwa kujipanga kwani soko la biashara mtandao  lipo mikononi mwao.

“Ndani ya Nchi tuna matawi 350 hivyo kama watajipanga katika biashara ya mitandaoni soko lipo mikononi mwao tunatakiwa kuwa wabunifu kutoka na teknolojia tuliyonayo,”amesema.

Mhandisi Kundo amesema uzinduzi wa duka hilo ni matokeo ya maendeleo ya Teknolojia pia inakuja kutatua changamoto ya  ugonjwa wa UVIKO 19.

Amesema duka hilo la posta mtandao litarahisishia wananchi waliopo maeneo ya pembezoni kupata huduma kwa haraka na kwa urahisi ambapo pia  italeta tija na kuongeza kipato kwa wananchi.

Kwa upande wake,Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk. Zainabu Chaula ameeeleza kuwa kazi ya wizara ni kuweka miundombinu itakayoiwezesha  nchi kwenda  kwenye Tanzania ya kidigital na kuwaomba wananchi kutumia huduma za posta kwani ni salama.

“Nafurahi kuona tuna mafanikio umoja ni nguvu  na ndio ambao utatuvusha kwani sisi tunatembea katika umoja,”amesema

Naye,Kaimu Posta Masta Mkuu, Macrice Mbodo amesema kutokana na badiliko makubwa ya Teknolojia  ambayo yanaenda kwa kasi kubwa dunia shirika la posta limekuwa  likifanya  mageuzi na maboresho katika  utoaji wa huduma zake  ili kuendana na sera za Umoja wa mashirika ya posta duniani.

Amesema kupitia uzinduzi rasmi wa duka hilo,wamekuja na huduma mpya tatu ambazo ni Posta Kiganjani, Vituo vya Huduma kwa wateja Pamoja na Duka Mtandao. 
Mbodo amesema huduma hiyo inategemea zaidi ushirikiano wa watanzania na kwamba  iwapo wizara na taasisi zote zitafungua vituo vya huduma pamoja posta ni wazi huduma nyingi wanazotoa zitapatikana kwa urahisi na kuongeza mapato yatayosaidia kukuza uchumi na kuondoa utegemezi.
“Kupitia huduma ya duka mtandao ambayo inasimamiwa na shirika la Posta Tanzania tumefanikiwa kupata zaidi ya Sh.milioni 300 huku Watanzania wengi wakiendelea kujisajili kutumia huduma hii, juhudi zetu ni kuhakikisha Watanzania wengi wanajiunga na duka mtandao ili kufanya biashara zao kwa gharama ndogo,”amesisitiza.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania,(TCRA) Dk Jabir Bakari,amesema sekta ya posta imepita katika changamoto nyingi ambapo amedai TCRA imetoa leseni 119 katika sekta ya Posta.