Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  Majaliwa  (kushoto) wakimfariji, Mwenyekiti wa Chama cha TLP  Taifa, Augustine Mrema ambaye Septemba 16, 2021    alifiwa na mkewe , Rose Mrema. Walikwenda nyumbani kwa Mheshimiwa Mrema eneo la Kiraracha Moshi, Septemba 23, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa TLP Taifa, Augustine Mrema na wanae  wakati alipokwenda nyumbani kwa Mwenyekiti huyo eneo la Kiraracha Moshi, Septemba 23, 2021 kuhani msiba wa Mke wa Mheshimiwa Mrema, Rose kilichotokea Septemba  16, 2021. Watoto  hao ni Peter Mrema (kulia), Kelekensia Mrema (wa pili kulia), Mary Mrema (wa tatu Kulia) na Michael Mrema (wa tatu kushoto)(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza waombolezaji wakati alipokwenda  nyumbani kwa Mwenyekiti wa TLP Taifa, Agustine Mrema, eneo la Kiraracha Moshi, Septemba 23, 2021 kuhani msiba wa Mke wa Mwenyekiti huyo, Rose Mrema aliyefariki Septemba 16, 2021. Wa pili Kulia ni  Mke wa Waziri Mkuu,  Mary Majaliwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)