Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali na afya Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catheline Katele akitoa neon la shukrani kwa wajumbe mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu ambapo ameweza kuibuka mshindi kwa kupata kura 48 dhidi ya 51 ambazo zimepigwa.
Baadhi yaw a sekretarieti ya Tughe Mkoa wa Pwani wanatekeleza majukumu yao ipasavyo katika uchaguzi huo ambao umefanyika katika ukumbi wa mikutano kwa Mkuu wa Mkoa.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo mkuu kutoka Wilaya mbali mbali za Mkoa wa Pwani wakiwa wametulia kusikiliza maelekezo ambayo yalikuwa yanatolewa na msimamizi wa uchaguzi ambaye hayupo pichani.
Mwenyekiti wa Tughe Mkoa wa Pwani wa kwanza kushoto akiwa amesimama na baaadhi ya viongozi wengine ambao wamechaguliwa katika uchaguzi huo mkuu.
mmoja wa mjumbe ambaye amechaguliwa kwa kupata kura 32 katika nafasi ya mkutano mkuu ngazi ya Taifa Dr. Michael Benedict akizungumza nje ya ukumbi na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na mikakati yake aliyojiwekea.
…………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, PWANI
CHAMA cha wafanyakazi wa serikali na afya Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Pwani umefanya uchaguzi wake mkuu na kufanikiwa kupata safu ya viongozi wapya katika nafasi mbali mbali huku Mwenyekiti wake akiibuka kuwa ni Catheline Katele ambaye atapata fursa ya kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Katika uchaguzi huo ambao ulifanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani uliweza kuhudhuliwa na wajumbe mbali mbali kutoka katika Wilaya zote saba uliweza pia kusimamia na afisa kazi wa Mkoa wa Pwani ambapo mwenyekiti huyo aliweza kuibuka na ushindi baada ya baada ya kupata kura 48 dhidi ya 51 ambazo zilizopigwa na mpinzani wake Dr. Alphonce Moyo akipata kura tatu.
Uchaguzi huo ambao uliendeshwa kwa amani na utulivu kutokana na wajumbe wote ambao walifika katika zoezi la upigaji kura kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote hivyo kupelekea uchaguzi huo kumalizika kwa hali ya utulivu.
Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti huyo wa mpya wa Chama cha wafanyakazi wa serikali na afya Tanzania (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catherine Katele amemeweza kuwashukuru wajumbe wote ambao wamemchagua na kuahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kila Nyanja lengo iikiwa ni kuwaletea maendeleo na kuwapambania katika mambo mbali mbali ya msingi.
Pia Mwenyekiti huyo alisema kwamba ataendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais wa awamu ya sita Mama Samia Suluhu Hassan katika kupambana na changamoto mbali mbali zinazowakabili wafanyakazi ikiwemo kupatiwa stahiki zao zote kwa mujibu wa sheria na taratibu ikiwemo kupandishwa madaraja pamoja na mishahara.
“Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu kwa siku ya leo nimeweza kupata fursa hii ya kuchaguliwa tena katika kipindi cha miaka mitano lakini kitu kikubwa nitahakikisha kwa upande wangu ninashirikiana na viongozi wenzangu katika kuweka mipango mizuri ambayo itawasaidia wafanyakazi kuweza kupata stahiki ikiwemo mupandishwa madaraja pamoja na mishahara.
Aidha Katele alisema kwamba anatambua wafanyakazi wa Mkoa wa Pwani baadhi yao bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali hivyo jambo hilo kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Mama Samia Suluhu Hasan linafanyiwa kazi katika ngazi mbali mbali lengo ikiwa ni kuwapa wafanyakazi stahiki zao kwa wakati.
Pia katika hatua nyingine aliongeza kuwa ataendelea kufanya kazi kwa weledi na msimgi iliyowekwa kwa kuzingatia sharia na taratibu zote na kubainisha kuwa atakuwa mzalendo katika kuwatumikia wafanyakazi wote bila ya upendeleo na ubaguzi wowote kwa maslahi ya Taifa.
Naye mmoja wa mjumbe ambaye amechaguliwa kwa kupata kura 32 katika nafasi ya mkutano mkuu ngazi ya Taifa Dr. Michael Benedict amebainisha mipango yake ambayo ataipambania kwa hali na mali kwa lengo la kuweza kushirikiana na viongozi wenzake kwa ajili ya kuleta mbadailiko chanya ya kimaendeleo pasipo ubaguzi wowote.
Kwa upande wake aliyeshinda katika nafasi ya mwakilishi wa vijana Mkoa wa Pwani Violeth Mahundi ambaye aliibuka kwa kupata kura 42 kati ya 51 zilizopigwa na kuahidi kuweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia vijana waweze kutambua wajibu wao, haki na sheria za kazi na kuwaasa kachana na tabia ya utumiaji wa madawa ya kulevya.
UCHAGUZI huo wa Tughe Mkoa wa Pwani umesimamiwa na afisa kazi Mkoa wa Pwani Razina Tunga ambapo nafasi mbali mbali ziliweza kuchgaliwa zikiwemo za nafasi ya Mwenyekiti, nafasi za wajumbe wane wa mkutano mkuu Taifa,nafasi wajumbe watatu wa kamati ya utendaji ngazi ya Mkoa,mjumbe wa baraza kuu,mwakilishi wa walemavu, mwakilishi wa vijana pamoja na nafasi mbali mbali.