Mwanasheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)Lupakisyo Mwambinga akifafanua gharama za tozo ya mirabaha zilizopendekezwa katika kanuni mpya ya Leseni na Utangazaji ya mwaka 2021 katika kikao cha kutoa maoni kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari wa Nyanda za Juu Kusini kilichofanyika leo Agosti 09,2021 Jijini Mbeya .
Mmiliki wa GMCL FM Brown Kikoti akitoa maoni ya Kanuni ya Leseni na Utangazaji ya Mwaka 2021 ambapo ameomba COSOTA kupunguza tozo ya mirabaha kwa vyombo vya habari mpaka shilingi laki tano au tatu kutoka kiasi cha shilingi milioni moja iliyopendekezwa leo Agosti 09,2021 Jijini Mbeya, mara baada ya wasilisho la kanuni hiyo lililofanywa na Mwanasheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Lupakisyo Mwambinga (hayupo pichani).
Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mhandisi Alinanuswe John akiwapongeza wamiliki wa vyombo vya habari nyanda za juu kusini (hawapo pichani) leo Agosti 09,2021 kwa kushiriki kikao cha kutoa maoni ya Kanuni ya Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa Umma ya 2021 kilichofanyika leo Agosti 09,2021 Jijini Mbeya, chenye mapendekezo ya gharama ya tozo za mirabaha ya wasanii wa muziki kutoka vyombo vya habari .
Mmiliki wa Kyela FM Denis Mlowe akitoa maoni yake leo Agosti 09,2021 kwa Kanuni ya Leseni na Utangazaji ya mwaka 2021 ambapo ameomba COSOTA kuadaa utaratibu wa chombo kuamua inapiga muziki wa wasanii gani tu , mara baada ya wasilisho la kanuni hiyo lililofanywa na Mwanasheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)Lupakisyo Mwambinga (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Jijini Mbeya.
Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nyanda za Juu Kusini wakimsikiliza Mwanasheria wa COSOTA alipokuwa akiwasilisha mapendekezo ya tozo ya mirabaha kwa vyombo vya habari yaliyoainishwa katika Kanuni Mpya ya Leseni na Utangazaji ya mwaka 2021 katika kikao cha kutoa maoni kilichofanyika leo Agosti 09,2021 Jijini Mbeya.
Mwanasheria wa Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Lupakisyo Mwambinga (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa Vyombo vya Habari Nyanda za Juu Kusini mara baada ya kikao cha kukusanya maoni ya mapendekezo ya tozo ya mirabaha kwa vyombo vya habari kutoka katika Kanuni Mpya ya Leseni na Utangazaji ya mwaka 2021, kilichofanyika leo Agosti 09,2021 Jijini Mbeya, wa kwanza kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mhandisi Alinanuswe John.
****************************
Na Anitha Jonas – COSOTA, Mbeya
10/08/2021
Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) ya ahidi kuzingatia maoni ya yaliyotolewa na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nyanda za Juu Kusini katika Kanuni mpya za Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa umma.
Kauli hiyo imetolewa Leo Jijini Mbeya na Mwanasheria wa COSOTA Lupakisyo Mwambinga mara baada ya kueleza lengo la kuundwa kwa Kanuni hizo na kuwapitisha wadau hao.
“Pamoja na kwamba mtakuwa mnatoa maoni kwa kuzungumza naomba pia mjaze fomu ya maoni ili tuweze kupata maoni yenu na kwa njia ya maandishi kila mmoja ajaze fomu hiyo tutahakikisha tunazingatia maoni yote mtakayotoa,”alisema Mwambinga.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho cha wadau Mwanasheria huyo wa COSOTA alisisitiza kuwa sheria ya Hakimiliki nchini inaeleza wajibu wa watumiaji wa kazi za Muziki kulipa Mirabaha hivyo suala la ulipaji wa tozo hiyo siyo la kisiasa.
Kwa upande wa Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mhandisi Alinanuswe John amewapongeza wamiliki wa vyombo vya habari Nyanda za Juu Kusini kwa kushiriki kikao hicho, na kuwasihi wazungumze kwa hoja na waache kuwa na hasira wanapochangia hoja sababu kikao hicho kimelenga kuweka mazingira rafiki ya ulipaji wa tozo hiyo ya mirabaha.
Pamoja na hayo nae Muwakilishi wa Mmiliki wa Hekima FM Innocent Patrick kutoka Mbinga aliomba COSOTA kushusha tozo hiyo ya mpaka kiasi cha shilingi laki tano au laki tatu, sababu kwa sasa hali ya kiuchumi ni ngumu kutokana na wimbi la UVIKO 19.
Halikadhalika nae Muwakilishi wa Mpanda Redio Denis Kakala ameiomba COSOTA kuweka aina ya Muziki ambayo ikichezwa ndiyo inalipiwa huku akisema rate card za matangazo hazina uhalisia katika malipo ya matangazo yanayochezwa katika vituo vya vyombo habari.
Katika hitimisho la kikao hicho Mwanasheria huyo alisema kuwa ameiona changamoto ya wadau hao kutokuwa na elimu ya kutoka kuhusu ulipaji wa mirabaha hivyo COSOTA itakipanga kuja kutoa elimu .
COSOTA imeomba wadau hao katika kikao kijacho ni vyema waliyohudhuria kikao hicho ndiyo waje kikao kijacho badala ya kumtuma mtu mwingine kwani hiyo inaleta changamoto na kuanza upya kuelezana yaliokwisha kujadiliwa.