Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akilakiwa na wananchi wa kijiji cha
Burugo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambako
yuko kwenye ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF na
kukutana na Watumishi wa Umma kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na wananchi na
Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Burugo
(hawapo pichani) juu ya utekelezaji wa miradi ya TASAF.
Baadhi ya Wananchi na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
katika katika kijiji cha Lukindo kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
Mkoani Kagera wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
(hayupo pichani).
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (katikati) akiwa nyumbani kwa
mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Burugo Bi. Justa Migini
(kulia kwa Naibu Waziri),wa kwanza kushoto ni Meneja wa Miradi ya Ajira
za Muda TASAF Bw. Paul Kijazi wakishuhudia nyumba iliyojengwa na
mlengwa huyo kwa kutumia ruzuku ya TASAF.
************
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amewataka wanufaika wa Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini ambao wana nguvu za kufanya shughuli
mbalimbali za maendeleo wafanye hivyo, ili waweze kujiingizia kipato
badala ya kutegemea ruzuku kutoka Serikalini kupitia TASAF.
Dkt. Mwanjelwa ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza na
wananchi na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika vijiji
vya Lukindo na Burugo, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.
Dkt. Mwanjelwa amesema utawekwa utaratibu maalum ambao kila
mwananchi mwenye uwezo wa kufanya kazi ambaye yuko kwenye Mpango
wa Kunusuru Kaya Maskini afanye hivyo na kulipwa ujira kutokana na kazi
atakayoifanya.
“Ni wajibu wa walengwa wote wenye uwezo wa kufanya kazi ambao wako
kwenye mpango huu, wafanye kazi badala ya kutegemea ruzuku ili nguvu
kazi yao isipotee bure,” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Ameongeza kuwa, kufanya kazi kwa wanufaika hao ni sehemu ya
kuwasaidia katika kuboresha maisha yao na kusisitiza kuwa ruzuku itabaki
tu kwa wananchi wasioweza kufanya kazi ambao wengi wao ni wazee na
watoto.
Aidha Naibu Waziri huyo amewataka wataalam wa halmashauri za wilaya
nchini kote kuhakikisha kuwa wanafanya ufuatiliaji wa karibu kwa
wanufaika ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na tija kubwa.
Dkt. Mwanjelwa anaendelea na ziara ya kikazi mkoani Kagera kukagua
utekelezaji wa shughuli za TASAF na kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi
2
wa Umma katika Halmashauri zote za mkoa huo ambapo tayari
ameshatembelea Manispaa ya Bukoba na Halmashauri ya Bukoba Vijijini.