Kamisha Mkuu wa TRA Alfayo Kadata akizugumza na wafanyabiashara jijini Arusha.picha Happy Lazaro)
Mkuu wa Mkoa Arusha, John Mongela akizungumza na wafanyabiashara jijini Arusha.(Happy Lazaro).
****************************
Happy Lazaro,Arusha 
Mamlaka ya mapato Tanzania imetangaza kuanza kutumia sheria katika kutoa adhabu kwa wale wote watakao kaidi kutoa au  kudai risiti kwakuwa wamekuwa wakichangia upotevu wa mapato ya serikali  hali inayodidimiza uchumi na  kukosa maendeleo ya nchi.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)  Alphayo Kidata ameyasema hayo katika mkutano  wa TRA  na   walipa  Kodi  Jiijini  Arusha wakiwemo wafanyabiashara pamoja na wakuu wa Taasisi mbalimbali .
” Kuanzia Sasa tutatumia Sheria zetu kutoa adhabu Kali kwa wale wasiotoa risiti no vizuri tuwe na utamaduni wa kudai risiti kwani endapo utabainika itachukuliwa hatua kali “amesema 
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela akizugumza katika mkutano huo , amewataka wakazi wa mkoa wa Arusha kushirikiana katika kufichua biashara ya bidhaa bandia ambazo zimekuwa zikichangia kudidimiza uchumi .
“Bado Mkoa wetu unatumika Kama daraja la bidhaa za kughushi kwa  hiyo sisi Kama Mkoa wa Arusha tunatakiwa kushirikiana na Kuendelea kuhamasisha kuepuka kufanya biashara za bidhaa za kughushi “amesema 
Naye Mmoja wa washiriki  wa mkutano huo Kelvin Remen amesema  mkutano huo ni  jukwaa muhimu litakalo wasaidia wafabishara kulipa kodi kwa njia rafiki bila kuwa na matatizo yeyote kwa wafanyabiashara.
“Hii ni fursa kwa walipa Kodi kupata nafasi ya kukaa na uongozi wa juu wa  TRA ilinkuwaeleza Changamoto zetu ili kuweza kufikia malengo yetu na Taifa pasipo kumwumiza mfanyabiashara yeyote “alisema 
Mkutano huu wa siku mbili Kati ya TRA na walipa Kodi umelenga kuinua uchumi na kuimarisha matumizi sahihi mashine za kielekroniki   kwa wafanyabiashara na wateja hasa katika kuinua uchumi wa Nchi .