Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Maadhimisho ya Sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwenye ukumbi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu hicho, jijini Dar es salaam, Mei 24, 20921. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu yakiyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. william Anangisye akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu yakiyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Amosi Makala akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu yakiyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo na Utafiti Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof Bernadeta Kilian akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu yakiyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
Wadau mbalimbali wa tafiti na ubunifu wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu yakiyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
*********************************
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa amewataka watafiti na wabunifu nchini kuongeza kasi ya kufanya tafiti ili nchi iende sambamba na mabadiliko yanayotokea ulimwenguni kote.
Ametoa wito huo leo Mei 24, 2021 wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya sita ya wiki ya utafiti na ubunifu yakiyofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
“Mabadiliko haya ya teknolojia yanatokea kwa kasi kubwa ulimwenguni yanachochewa na mwenendo wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hivyo basi, nasi hatunabudi kujipanga vyema ili kuendana na kasi hiyo”.
Amesema kuwa ni lazima watafiti na wabunifu katika sekta zote wachukue hatua za makusudi katika kubuni na kutumia teknolojia zinazoibuka kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu ya viwanda na jamii yetu.
“Wakati tukifanya hayo yote, ni muhimu pia kujitayarisha kutumia kikamilifu matokeo ya tafiti zetu kama fursa au bidhaa adimu ya biashara”
Aliongeza kuwa baada ya tafiti hizo wahakikishe matokeo ya tafiti yanapelekwa kwa umma ili uweze kufaidika na matokeo hayo kwa kupata suluhisho za changamoto mbalimbali zinazoikabili Jamii badala ya kuyafungia makabati.
Aidha, Waziri Mkuu amevitaka vyuo vikuu vyote nchini kuweka utaratibu wa kufanya utafiti na kisha kuonesha matokeo ya tafiti ili kusaidia kuimarisha uhusiano wa karibu baina ya vyuo na soko la ajira.
Kadhalika Waziri Mkuu ametoa wito kwa wenye viwanda kutoa ufadhili wa tafiti na bunifu zinazohusiana na bidhaa zinazozalishwa katika viwanda vyao.
“Tumieni vizuri wataalamu wa vyuo vyetu kwani wanaweza kuleta majibu ya changamoto mbalimbali katika uzalishaji bidhaa, masoko ya bidhaa, mahitaji ya wateja na mambo mengine mengi”
Pia, Waziri Mkuu amekitaka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kutekeleza mpango wa vitengo vya utafiti kwenye mikoa ikiwemo cha mkoa wa Lindi ambako tayari walikwisha pewa eneo.
Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha tafiti ili taifa liweze kunufaika na teknolojia ya kisasa na kutoa huduma kwa jamii.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. william Anangisye amesema Chuo hicho kimekuwa kikitenga fedha kutoka katika vyanzo vyake vya ndani kwaajili ya utafiti na ubunifu ambapo katika mwaka huu wa masomo 2020/2021 kilitenga zaidi ya bilioni 2 kwaajili ya utafiti na ubunifu pia katika mwaka wa masomo 2021/2022 kimetenga bilioni 2.2 kwaajili ya utafiti na karibu bilioni 1.15 kwaajili ya ubunifu.
“Kwa idadi ya watafiti na wabunifu waliopo na mipango tulionayo ya kuongeza tafiti na ubunifu tuna tatizo la changamoto ya rasilimali fedha”. Amesema Prof.Anangisye
Pamoja na hayo Prof.Anangisye amesema kuwa kwa mwaka huu wana miradi mingi ya utafiti kutoka kwenye taaluma kuu zote za campas kuu na vyuo shiriki vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.