Prof.Mkenda amesema kuwa hivi sasa kipaumbele cha Wizara hiyo ni katika uzalishaji wa mbegu bora kupitia mashamba hayo ndio maana imejipanga
kuanzisha mfuko huo.
“Tutajitahidi katika hili kwa sababu tunaanzisha mfuko wa umwagiliaji tukipata fedha tutapeleka katika miradi inayoendelea na siyo kuanzisha
vitu vipya,”amesema Prof.Mkenda.
Ameeleza kuwa itasaidia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kutokana na kuagiza mbegu nje ya nchi ambapo serikali itajitahidi na ASA
kusimamia suala hilo.
Pia Prof.Mkenda amesema kuwa ipo haja ya serikali kuwa msimamo unaoakisi kauli mbiu ya kilimo ni uti wa mgongo ili wakulima walime kwa tija na kuondokana na umasikini miongoni mwao.
“Tunaweza kuwa na uchumi wa kati na hata kufikia uchumi wa juu lakini wimbi la umasikini likaendelea kwa wananchi na tukawa tegemezi wa chakula,lakini pia hatuwezi kuwa na mageuzi ya viwanda bila kufanya mageuzi ya kilimo hususani katika suala la mbegu,”amesema
Hata hivyo amesema kuwa ni lazima mashamba yote ya ASA yafufuliwe kwa kuwa utegemezi wa mbegu kutoka nje ya nchi wakati mwingine hausaidii kilimo cha hapa nchini.
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya ASA, Dk. Ashura Kihupi amesema kuwa zipo kero kubwa kwenye sekta ya mbegu ni uwekezaji mdogo uliofanywa na serikali, mtaji mdogo kwa ajili ya kuzalisha mbegu.
Dk.Kihupi amesema kuwa katika shamba la mbegu la Msimba lililopo wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro, hasara kubwa imetokea kwa sababu hakuna kilimo cha
umwagiliaji.