Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Rosalynn Mworia ,akizungumzia uzinduzi wa tovuti ya elimu iitwayo E- fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari vinavyofuata mitaala ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao leo Mei 7,2021 jijini Dodoma
Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekonolojia Prof. Joyce Ndalichako,akizungumza wakati akizindua tovuti ya elimu iitwayo E- fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari vinavyofuata mitaala ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao leo Mei 7,2021 jijini Dodoma
Baadhi ya wanafunzi waliohudhuria tukio hilo wakimsikiliza Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekonolojia Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati akizindua tovuti ya elimu iitwayo E- fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari vinavyofuata mitaala ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao leo Mei 7,2021 jijini Dodoma
Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekonolojia Prof. Joyce Ndalichako,akiwa na Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Rosalynn Mworia ,kushoto kwake ni Naibu Waziri wake Mhe.Omary Kipanga na kulia ni Katibu Mkuu wake Dk.Leonard Akwilapo, wakizindua tovuti ya elimu iitwayo E- fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari vinavyofuata mitaala ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao leo Mei 7,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekonolojia Prof. Joyce Ndalichako,akikabidhiwa zawadi na Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Rosalynn Mworia mara baada ya kuzindua tovuti ya elimu iitwayo E- fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari vinavyofuata mitaala ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao leo Mei 7,2021 jijini Dodoma
Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekonolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzia mara baada ya kuzindua tovuti ya elimu iitwayo E- fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari vinavyofuata mitaala ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao leo Mei 7,2021 jijini Dodoma
………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
KAMPUNI ya Vodacom Foundation imezindua tovuti ya elimu iitwayo E- fahamu yenye lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi kupata vitabu vya ziada na kiada kwa shue za msingi na sekondari vinavyofuata mitaala ya kutoka maktaba ya Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao.
Akizungumza wakati akizindua tovuti hiyo katika mashindano ya Sayansi ,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) 2021 Waziri wa Elimu,Sayansi na Tekonolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema,kwa kupitia tovuti hiyo wanafunzi watajifunza masuala ya masomo zaidi wanapotumia simu za mkononi.
Lengo la Tovuti hiyo pia ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi na sekondari nchini.
“Mtandao huu utaboresha elimu kwani italeta hamasa kwa wanafunzi kujisomea kutokana na wanafunzi wengi kupenda kutumia simu za mkononi .”amesema Prof. Ndalichako
Aidha Profesa Ndalichako amefurahishwa na kampuni hiyo ilivyoshirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote kutoa Komyuta na Routers kwa wanafunzi .
Prof.Ndalichako ameiomba kampuni hiyo kuongeza vitabu zaidi katika tovuti hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi kujifunza huku akitoa rai kwa kampuni nyingine kuiga mfano wa Vodacom Tanzania Foundation kutumia teknolojia kusaidia jamii.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Vodacom Foundation,Rosalynn Mworia amesema E- fahamu ni tovuti ya maswala ya kielimu inayopatikana mtandaoni bure kwa ajili ya wateja wa Vodacom huku akisema kampuni hiyo imeamua kutoa huduma hiyo bure kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kutoa elimu bila malipo kwa shule msingi na sekondari nchini.
Bi.Mworia amesema tovuti hiyo ina nyenzo na taarifa muhimu za kielimu kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ikijumuisha masomo ya Hisabati,Sayansi,Sanaa na Sayansi ya Jamii.
“Ili kupata E- fahamu kwenye simu ama Kopyuta utahitaji kuunganishwa na huduma ya mtandao wa internet ya Vodacom au kutumia WiFI ambapo baada ya hapo mhusika ataweza kuangalia video za mafunzo ambapo amesema maudhui yanapatikana katika lugha za Kiswahili na Kiingereza ambapo yapo katika muundo wa sauti,video,machapisho ya PDF na mazoezi shirikishi.”amesema Mworia
Mworia amesema tovuti hiyo imeanza mwaka 2017 na tayari wamewafikia
jumla ya wanafunzi wapatao 150,000.