Mchungaji Rehema Gwao wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kati , akisaini katika kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli. |
Viongozi wa dini wakisubiri kusaini katika kitabu hicho.
Viongozi wa dini wakisubiri kusaini katika kitabu hicho.
Mchungaji Wilson Mkoma wa Kanisa la EAGT-Puma na Katibu CPCT Mkoa wa Singida akitoa salamu za rambirambi.
Mjumbe wa Baraza la Mashehe Mkoa wa Singida, Issa Nassoro (kushoto), akizungumzia jinsi alivyo mfahamu Rais Magufuli
UMOJA wa Dini mbalimbali mkoa wa Singida, umepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati
John Pombe Joseph Magufuli kilichotokea majira ya saa 12:00 jjionu, tarehe
17/03/2021, katika Hospitali Nzela Dar es Salaam.
Katika salamu zetu za rambirambi tunatoa pole kwa mama Mjane Janeth
J.P.Magufuli), watoto wa marehemu, ndugu jamaa na marafiki, aliyekuwa makamu wa
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na watanzania wenzetu, na afrika kwa
ujumla.
Tunawaomba watanzania wote hususani walioko Mkoa wa Singida, kuwa na
utulivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wetu,
shujaa wa Afrika. tunaamini kuwa Mungu alitupa zawadi na ni Mungu huyu huyu
ameamua kumtwaa kutoka katika maisha haya sasa na mapenzi yake. tunawasihi
watanzania wote kuiombea nchi ili idumu katika upendo, amani, utulivu na
mshikamano huku tukisahau tofauti ztu na kusonga mbele kuyaenzi na kuyaendeleza
mazuri yote aliyotuachia. pia tumuombee rehema marehemu ili afike mbinguni
salama.
RAI:
Tunatoa rai kwa wote wasioitakia mema nchi yetu waliokonndani na nje ya
nchi kwamba wasifikirie kuwa kuondokewa na Rais ni fursa kwao kuharibu upendo,
amani, utulivu na mshikamano uliojengwa na waasisi wetu kwa muda mrefu. Mungu
atuepushe na wote wenye kulitakia mabaya Taifa letu. pia tunamuombea mama yetu
mpendwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kama
lilivyo jina lake: Samia mwenye kusikia, atakuwa msikivu kwa Mungu na kwa
wanadamu. Suluhu – kufanya suluhu/upatanisho mahali ambapo hakuna amani na
Hassan maana yake kutenda mema yote aliyoyaanzisha mtangulinzi wake. mungu
amvuvie Roho wake na kumvika ujasiri, akasimame kiume kwa nguvu za Mungu
kuliongoza Taifa hili pasipo hofu, mashaka wala tashwishi ya aina yoyote, maana
Mwenyezi Mungu atakuwa naye siku zote za uongozi wake.