Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt Zainab Chaula akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za muungano ambazo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kilichofanyika tarehe 8.3.2021 visiwani Zanzibar
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Amour Bakari akizungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za muungano ambazo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kilichofanyika tarehe 8.3.2021 visiwani Zanzibar
Baadhi ya watendaji walioshiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za muungano ambazo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kilichofanyika tarehe 8.3.2021 visiwani Zanzibar wakichangia ajenda mbalimbali zilizowasilishwa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation), Bw. Waziri Kindamba(kushoto), Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba waliposhiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya (JMT) na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ) kilichofanyika tarehe 8.3.2021 visiwani Zanzibar
Baadhi ya watendaji walioshiriki kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara za muungano ambazo ni Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT) na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kilichofanyika tarehe 8.3.2021 visiwani Zanzibar
……………………………………………………………………………………………
Na Faraja Mpina – WMTH, Zanzibar
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula amewataka watendaji wa taasisi za mawasiliano zenye matawi Tanzania bara na visiwani kuwa wazi kwa wananchi kwa kutoa maelezo ya kina kuhusu sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ili kuondoa sintofahamu kwa huduma zinazotolewa na taasisi hizo zilizo katika pande zote mbili za muungano ambazo ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na Shirika la Posta Tanzania (TPC).
Hayo ameyazungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT)na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kilichofanyika tarehe 8.3.2021 visiwani Zanzibar.
Dkt. Chaula ameongeza kuwa, taasisi hizo zinatakiwa kuzifahamu, kuzielewa na kuzifanyia kazi sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya utoaji wa huduma wanazozitoa ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii kufuata sheria hizo bila shurti.
“Tulikuwa na hoja nane baada ya kuzichambua zimebaki tano, ambapo kimsingi ni masuala ya kuweka sawa kanuni, taratibu na sheria zetu pamoja na kuongeza uelewa kwasababu lengo kuu la kuzitunga ni kuhakikisha kuwa zinafuatwa”, Dkt.Chaula
Aidha, amesema kuwa kikao kilikuwa kizuri na wataalamu walijipanga vema katika kufanya wasilisho ambapo changamoto mbalimbali zilizowasilishwa zimechukuliwa na kuboreshwa na zitawasilishwa katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hizo mbili kwa lengo la kuzifahamu na kuzitolea maamuzi ili wananchi waendelee kufurahia muungano.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ) Amour Bakari amesema kuwa kikao hicho ni muendelezo wa vikao vya mashirikiano baina ya taasisi za mawasiliano za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambavyo awali vilianza katika ngazi ya watendaji.
“Kikao cha leo ni cha ngazi ya Makatibu Wakuu, na yale yote yaliyojadiliwa katika kikao hiki yatapelekwa katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hizi mbili kitakachofanyika siku ya alhamisi ya tarehe 11.3.2021 hapa Zanzibar”, Amour Bakari
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari