Mtaalam kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nuru Lugawa akimpima uzito na urefu mchezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Mohamed Mbarak wakati wachezaji wa timu hiyo walivyofika JKCI kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi mwezi huu.
Mtaalam wa maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jesca Mlay akimtoa damu mchezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Abdul Libandika kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wachezaji 24 wa timu hiyo walipofika katika taasisi hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi huu.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gudila Swai akimpima shinikizo la damu mchezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Silverster Otto wakati wachezaji wa timu hiyo walipofika JKCI kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi huu.
Fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jasmin Keria akimpima mfumo wa umeme wa moyo unavyofanya kazi (Electrocardiography – ECG) kapteni wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys Ladaki Chasambi wakati timu hiyo ilipofika JKCI kwa ajili ya kuwafanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo kabla ya kushiriki mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Morocco katikati ya mwezi huu.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa chini ya miaka 17 Serengeti Boys wakisubiri kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Wachezaji 24 wa timu hiyo walifanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi, umeme wa moyo unavyofanya kazi na damu ikiwa ni mojawapo ya kutekeleza sheria ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa kila mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kupima.
Picha na: JKCI