Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe akizungumza katika tuzo kwa viwanda vikubwa na vidogo vinavyofanya kazi kwa kuzingatia falsafa ya KAIZEN yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kaimu Balozi japan nchini Nirinuma Takashi katika tuzo kwa viwanda vikubwa na vidogo vinavyofanya kazi kwa kuzingatia falsafa ya KAIZEN yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
katika tuzo kwa viwanda vikubwa na vidogo vinavyofanya kazi kwa kuzingatia falsafa ya KAIZEN yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Mkurugenzi idara ya maendeleo ya viwanda kutoka wizara ya viwanda na biashara Ramson Mwilangali akizungumza katika tuzo kwa viwanda vikubwa na vidogo vinavyofanya kazi kwa kuzingatia falsafa ya KAIZEN yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof.Riziki Shemdoe akitoa tuzo kwa washindi katika tuzo kwa viwanda vikubwa na vidogo vinavyofanya kazi kwa kuzingatia falsafa ya KAIZEN yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Wizara ya viwanda na biashara Prof..Riziki Shemdoe akipata picha ya pamoja na baadhi ya washindi katika tuzo kwa viwanda vikubwa na vidogo vinavyofanya kazi kwa kuzingatia falsafa ya KAIZEN yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
*********************************************
KATIKA kuhakikisha falsafa ya KAIZEN inatekelezwa katika sekta mbalimbali nchini ikiwemo viwanda katika kuleta tija na maendeleo ya Taifa Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya KAIZEN Afrika yatakayofanyika mwezi Juni mwaka huu na kuhudhuria na nchi 16 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya pili ya KAIZEN Tanzania yaliyoambatana na utoaji tuzo kwa viwanda vikubwa na vidogo vinavyofanya kazi kwa kuzingatia falsafa ya KAIZEN, Katibu mkuu wa Wizara ya viwanda na biashara Prof.Riziki Shemdoe amesema serikali imekuwa ikitenga fedha za kuendeleza miradi inayotekelezwa kupitia falsafa ya KAIZEN kwa kushirikiana na Serikali ya Japan ambao ni wafadhili wa KAIZEN katika kuendeleza viwanda.
“Wizara ya viwanda na biashara imekuwa ikisimamia maendeleo ya biashara, viwanda vikubwa na vidogo pamoja na sera rafiki zinazoendana na wakati na tupo katika mchakato wa kuweka sera mpya na za kitaifa katika masuala ya kumlinda mlaji, haki miliki na ubora was bidhaa ambao utaleta ushindani katika soko la kidunia.” Amesema Prof.Shemdoe.
Pia amewataka washiriki wa mkutano huo kuwa mabalozi bora wa falsafa ya KAIZEN katika utendaji kazi pamoja na kutumia fursa za ujio wa mataifa kumi na sita nchini.
“Hii ni fursa kwetu watanzania katika kuhakikisha tunakuza viwanda na biashara zetu, wakifika wageni tuwatembeze katika vivutio vyetu, tuwaoneshe bidhaa za viwanda vyetu pamoja na kubadilishana uzoefu wa masoko.” Amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi idara ya maendeleo ya viwanda kutoka wizara ya viwanda na biashara Bw.Ramson Mwilangali amesema, maadhimisho ya KAIZEN nchini yamelenga kubadilishana uzoefu, fursa na kupata maoni kutoka kwao wadau mbalimbali kuelekea maadhimisho ya KAIZEN Afrika yatakayofanyika nchini.
Mwilangali amesema Licha ya falsafa ya KAIZEN kuwa ngeni miongoni mwa umma wa watanzania elimu bado inaendealea kutolewa zaidi kwa sekta mbalimbali.
Vilevile kaimu Balozi wa Japan nchini Nirinuma Takashi amesema Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha miradi mingi zaidi ya kujenga Taifa inatekelezwa Tanzania.
Ameeleza kuwa uendelezaji wa viwanda vidogo ni muhimu katika kujenga uchumi wa nchi na kuwataka washiriki na washindi wa Tuzo za KAIZEN kuwa mabalozi katika kutangaza falsafa hiyo katika maeneo yao ya kazi.
Maadhimisho hayo yameenda sambamba na utolewaji wa vyeti kwa viwanda 18 vilivyoshiriki pamoja na zawadi kwa viwanda vilivyofanya vizuri zaidi kwa kuzingatia falsafa ya KAIZEN ambavyo ni pamoja na Quality Form (Dar es Salaam,) New Kingdom (Mbeya,) Kioo Limited, Super Doll na Maswa Nutrition kutoka Simiyu.
KAIZEN ni neno la kijapani lenye maana ya ‘badilika’ kwa ubora/uzuri na hutumika katika biashara, KAIZEN huusu shughuli endelevu zinazofanyika ili kuboresha kazi, mfumo, michakato na nyanja zote za kuendesha biashara.