Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WATANZANIA wametakiwa kuulinda, kuu­enzi na kuuendeleza Muungano wa Tanzania kwa kuwa ni tunu ya taifa na msingi wa maendeleo ya wananchi wa pande zote mbili za Muungano.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Juma Mohamed Salum, Novemba 25, 2026, wakati wa mahojiano maalumu katika kipindi cha Hello Tanzania kinachorushwa na Redio Uhuru FM.

Alisema Muungano wa Tanzania umejengwa katika misingi ya umoja, undugu, kuheshimiana na mazungumzo, misingi iliyowekwa na waasisi wake, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.