Happy Lazaro,Arusha .
Arudha .Wahitimu wametakiwa kutumia taaluma na ujuzi walioupata kwa ufanisi mkubwa sambamba na kutumia teknolojia vizuri ili kutatua changamoto za maisha ya wananchi na kuongeza kasi ya maendeleo nchini.
Hayo yamesemwa na Askofu msaidizi wa kanisa katoliki jimbo kuu la Dar es salaam Hennry MchaMungu wakati akizungumza katika mahafali ya Nane ya wahitimu wa ngazi mbali mbali wa chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino tawi la Arusha.
Amesema kuwa ,ni wajibu wetu kuhakikisha tunatumia vyombo vya mawasiliano vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa katika kukuza elimu na kuondokana na tabia ya kupotosha kwa kutumia mitandao hiyo vibaya.
Aidha amewataka kuhakikisha elimu waliyoipata ina leta manufaa makubwa kwao na wananchi kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu kwenye kazi zao sambamba na kutatua changamoto kwenye jamii.
Kwa upande wake Afisa uchumi kutoka benki ya BOT kanda ya Arusha Aristrides Mrema ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Gavana Mkuu wa BOT amewataka watoa huduma za kifedha nchini kuendelea kutoa huduma za kifedha kwa kufuata kanuni na sheria.
Aidha Mrema amewataka wasitoe huduma zenye masharti magumu yanayowaumiza watu kwani benki haitasita kuwachukulia hatua wale kali ikiwemo kuwanyanganya leseni wale wote watakaobainika kujihusisha na utoaji wa huduma za kifedha zinazowaumiza watu.
Naye Mkurugenzi wa chuo cha SAUT tawi la Arusha Fr. Dk Charles Rufyiriza amesema kuwa wao kama chuo wamewezesha wahitimu kupambana na changamoto za karne ya 21 .
“Sisi tumekuwa tukiwaandaa wanafunzi wetu kuweza kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ili waweze kuajirika ndani na nje ya nchi na kuweza kuwa watatuzi wazuri wa changamoto katika jamii.”amesema .
Wahitimu hao wameahidi kwenda kutumia taaluma waliyoipata kwa kuibua na kupatia uvumbuzi changamoto zinazoikabili jamii sambamba na kwenda kutoa ajira kwa wengine .



