Mkutano wa 46 wa Baraza la
Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Ngazi ya Wataalam umeanza jijini
Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano huo utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2024.

 

Pamoja na mambo mengine,
mkutano wa wataalam unajadili agenda mbalimbali muhimu kuhusu masuala ya
mtangamano wa Jumuiya hiyo ambazo baadaye zitawasilishwa kwenye Mkutano wa
ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa
kwenye Mkutano ngazi ya  Mawaziri.

 

Taarifa zilizopokelewa na
kujadiliwa ni pamoja na Taarifa ya utekelezaji wa maamuzi ya awali ya Baraza la
Mawaziri; Taarifa ya Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
Taarifa kuhusu masuala Forodha, Biashara na masuala ya kifedha; Taarifa kuhusu
Miundombinu, Sekta za Uzalishaji, Sekta za Kijamii na masuala ya Kisiasa;
Taarifa kuhusu masuala Fedha na Taarifa kuhusu Taasisi za Jumuiya.

 

Mkutano wa Ngazi ya
Wataalam umeongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji kutoka
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Haji
Janabi kwa niaba ya Mwenyekiti, Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya
mtandao

 

Mkutano huu wa ngazi ya
wataalam unafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba 2024 ukifuatiwa na
mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 26 Novemba 2024 na  tarehe 27 na 28 Novemba 2024 utafanyika
Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri ambao utapokea agenda mbalimbali kutoka kwa
Makatibu Wakuu .

 

Agenda zitakazojadiliwa
katika Baraza la Mawaziri zitawasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi
unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 Novemba 2024 kwa ajili ya kupitishwa na
kuridhiwa kwa utekelezaji.

 

Nchi nane Wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki za Burundi, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania na Uganda zinashiriki mkutano
huo.

 

Mkurugenzi
wa Kitengo cha Tathmini na Ufuatiliaji kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Haji Janabi akiongoza kikao kwa niaba ya
Mwenyekiti, Sudan Kusini ambao wameshiriki kwa njia ya mtandao. Kikao hicho cha ngazi ya wataalam  kimefanyika jijini Arusha kuandaa Mkutano wa 46 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 28 Novemba 2024. Kikao cha Wataalaam kitafanyika kuanzia tarehe 22 hadi 25 Novemba 2024 na kufuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu mnamo tarehe 26 Novemba 2024.M

Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji kutoka Wizara ya Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania, Bw. Benjamin Mwesiga akichangia jambo wakati wa kikao cha Wataalam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Abdilah Mataka akifuatilia kikao
Sehemu ya ujumbe wa Burundi wakishiriki Mkutano wa Wataalam
Ujumbe wa Kenya

 

Ujumbe wa Somalia

 

Ujumbe wa Uganda

 

Sehemu ya Wajumbe wakishiriki kikao cha wataalam

 

Sehemu nyingine ya wajumbe wakati wa kikao

 

Wajumbe wakishiriki kikao
 
Ujumbe wa Tanzania wakishiriki kikao

 

Kikao kikiendelea

 

Wajumbe wakati wa kikao

 

 

 

Kikao kikiendelea

 

Kikao kikiendelea