Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) uliofanyika leo Novemba 15,2024 jijini Dodoma.

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania  Bw.Tumaini  Nyamhokya,akielezea lengo la Mkutano Mkuu wa Nane wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) uliofanyika leo Novemba 15,2024 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani),wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) uliofanyika leo Novemba 15,2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete,akiteta jambo na Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania  Bw.Tumaini  Nyamhokya,wakati wa  Mkutano Mkuu wa Nane wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) uliofanyika leo Novemba 15,2024 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania Bw.Hery Hebert Mkunda,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Nane wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) uliofanyika leo Novemba 15,2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete,akiwa katika picha ya pamoja mara baaada ya kufungua  Mkutano Mkuu wa Nane wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) uliofanyika leo Novemba 15,2024 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Ridhiwani Kikwete,akisalimiana na watu mbalimbali mara baaada ya kufungua  Mkutano Mkuu wa Nane wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) uliofanyika leo Novemba 15,2024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna- DODOMA
WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali katika kupunguza makali ya maisha imeridhia taasisi za umma kuandaa mpango wa motisha kwa watumishi kulingana na tija na uwezo wa taasisi husika.
Hayo ameyasema leo  Novemba 15, 2024, jijini Dodoma wakati akifungua mkutano mkuu wa nane wa kazi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA) , Mhe. Kikwete amesema lengo la serikali ni kuendelea kuboresha maslahi ya wafanyakazi kadri uchumi wa nchi utakavyohimilika..
Aidha, amesema suala la uwiano wa kikokotoo kwa sekta ya umma na binafsi linazungumzika na tayari serikali imeelekeza Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa ajili ya kuangalia suala hilo.
 “Serikali haitavumilia ulegevu wa kuitishw vikao vya vyombo vya mashauriano hususan, LESCO, Bodi za Mishahara na Mabaraza ya Wafanyakazi kwa kuwa imeandaa rasilimali za kutosha kwa ajili ya vikao hivyo.”amesema Mhe.Kikwete
Aidha amesema kuwa Ofisi yake imeshaanza  mchakato wa kurejea sera ya ajira ambayo imesheeni mikakati ya kukuza ajira nchini.
Mhe.Kikwete amesema mkazo mkubwa umewekwa kwenye mazingira wezeshi kwa ajili ya vijana kujiajiri na kuwajengea uwezo wa kuajirika.
“Hapa tunazungumzia sera ya kazi ya kujitolea, sera za ajira za muda mfupi na mrefu, na sera inayotambua uwepo wa wenzetu waliosomeshwa vizuri lakini bado wanazurura hawana kazi,”amesema.
Hata hivyo  amekemea baadhi ya vyama ambavyo vimekuwa na migogoro ya uongozi na kwamba serikali inahitaji vyama imara vinavyoweza kushiriki kikamilifu na kwa weledi kwenye meza ya majadiliano
Naye, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania  Bw.Tumaini  Nyamhokya, ameshukuru serikali kwa ushirikiano wake na shirikisho huo katika kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi nchini.

 Bw.Nyamhokya amesema kuwa Mkutano Mkuu huu unaongozwa na Kauli Mbiu isemayo; “Ukuaji wa Uchumi wa Taifa, uthibitike katika hali Bora ya Maisha ya Wafanyakazi na Jamii”.

“Kauli mbiu hii inalenga kutambua na kuthamini kazi nzuri ya kuinua uchumi wa nchi iliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi madhubuti wa Rais wetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu  Hassan.”

Ameongeza kuwa ‘Tumeshuhudia juhudi kubwa za Serikali katika kuimarisha huduma za jamii nchini zikiwemo za Afya, Elimu, Miundo Mbinu ya Barabara na Nishati hivyo  TUCTA tunapongeza juhudi hizo.”

Hata hivyo amesema kuwa  umefika wakati sasa kwa Serikali kulitazama upya suala la mishahara ya Wafanyakazi wa Sekta zote na mazingira ya kazi kwa ujumla.

“Tunakumbusha kuwa kuboreshwa kwa maslahi ya wafanyakazi kuna mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Jamii kwa vile ni Soko la uhakikika la mazao ya Wakulima na bidhaa za Wafanyabiashara. Furaha ya Wafanyakazi ni kuona ukuaji wa uchumi unawaondoa kwenye umaskini wa kipato. “amesema 

Hata hivyo ameipongeza  Serikali kwa kusikiliza kilio cha Wafanyakazi na kukubali kuboreshwa kwa kikokotoo cha malipo ya mkupuo kwa Wastaafu.

“Hoja yetu hapa ni kuwa maboresho yanaonesha kunufaisha zaidi Sekta ya umma ambayo kiwango chao cha malipo ya mkupuo kimepanda hadi asilimia arobaini (40%) wakati kwa Sekta ya Binafsi kimeishia asilimia Thelathini na Tano (35%). Tofauti iliyopo kwenye uwiano huu inaleta hisia za upendeleo. TUCTA tunashauri milango ya mashauriano ifunguliwe ili jambo hili lijadiliwe na muafaka upatikane.”amesisitiza

Awali, akisoma risala Katibu Mkuu wa TUCTA, Hery Mkunda, ameshauri serikali irejeshe chombo cha kusimamia na kudhibiti mifuko ya hifadhi ya jamii
(SSRA) kwa kuwa wanaamini chombo hicho kina umuhimu mkubwa wa kusimamia mifuko ya hifadhi ya jamii.