Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, ndugu John Mongella, amewasili Kigoma na kufanya kikao-kazi na viongozi waandamizi na watumishi wa CCM mkoani humo, Septemba 21, 2024.
Katika kikao-kazi hicho, pamoja na mambo mengine, ndugu Mongella amesisitiza suala la kuendelea kujenga umoja na mshikamano ndani ya Chama.
Aidha, alisisitiza umuhimu wa utunzaji wa siri za vikao na maamuzi yanayofanywa ili kulinda usalama wa taarifa na kuhakikisha uaminifu ndani ya Chama.
Ndugu Mongella pia alikazia umuhimu wa kusimamia Katiba ya CCM, pamoja na kuzingatia kanuni, miongozo, na taratibu mbalimbali za Chama na Jumuiya zake.
Aliongeza kuwa utii na uzingatiaji wa misingi hiyo ni nguzo muhimu kwa viongozi na wanachama ili kuimarisha utendaji na kuhakikisha malengo ya Chama yanafikiwa kwa ufanisi.