Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo, ametembelea banda la Bodi ya Bima ya Amana katika maonesho ya Nanenane kitaifa jijini Dodoma. Akiwa katika banda hilo Mhe. Dkt. Jafo amepongeza kazi zinazofanywa na taasisi hiyo na kuwataka wananchi kuendelea kutunza fedha zao katika benki na taasisi za fedha wakiamini kwamba fedha hizo zinakingwa na Bodi ya Bima ya Amana endapo benki zao zitapata matatizo.

Katika banda hilo amepokelewa na Mkurugenzi wa Bodi ya Bima ya Amana, Bw. Isack Kihwili na Meneja Uendeshaji wa Bodi hiyo, Bw. Nkanwa Magina.